Na Bahati Hai
Dc, Hai Lazaro Twange, apewa kongole kwa kuandaa Bonanza Kwa lengo la kuhamasisha watu kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi
Wadau wa maendeleao Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro,wametoa kongole kwa Viongozi wa Wilaya hiyo kuona umuhimu wa kandaa bonanza kwa ajili ya kuhamasiaha Wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi ambalo uandikishaji umeanza October 11 hadi October 20 mwaka huu.
Haya yamejiri katika uwanja wa half London uliopo Bomang’ombe Wilayani humo kulikofanyika Bonanza hilo na kuhudhuria na Wadau mbali mbali wanaendelea pamoja na Viongozi wa Serikali
“Ni kweli tunnampongeza Mkuu wa Wilaya hiyo lazaro Twange pamoja na Viongozi wa Halmshauri kwa kuona umuhimu wa kuanda bonanza hilo, lengo likiwa ni kuhamasisha watu kujitokeza na kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi ili wawe na sifa ya kuchagua Viongozi “Wamesema Wadau hao
Shaaba Mwanga mmoja ya wadau hao, amesema leo walikuwa kwenye bonanza liliandaliwa Mkuu wa Wilaya hiyo na kwamba limefana kwa kiasi kikubwa
Mwanga amesema kubwa ambalo lilikuwa limejitokeza ni kuhamasisha watu kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi , ambapo ametumia michezo Kwa sababu ndiyo miongoni mwa sehemu inayokusanya watu wengi
Kwa maana ya vijana, wazee lakini na watu wa marika mbali mbali,bonanza limefana sana,michezo mbali mbali ikiwamo kukimbia kwa magunia,mbio fupi na ndefu lakini kumekuwa na michezo ya miguu timu mbali mbali kata 17 na washindi kupewa dawadi
Kwa hiyo tuwepongeze Viongozi hao wametumia frusa za michezo kama nilivyosema awali inakutanisha watu wa marika tofauti Kwa lengo la kuhamasisha watu kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi ili kuwa na sifa ya kuchagua Viongozi katika uchunguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu
Shaaba amesema Viongozi wa Serikali za mitaa ndiyo wanaoishi jirani zaidi na Wananchi,hivyo ni muhimu kushiriki katika kuwachagua wale watakaolunda maslahi ya jamii husika
Amesema upatikanaji wa viongozi wazuri unaanza Kwa kujiandikisha na baadaye kujitokeza kupiga kura
Awali Mkuu wa Wilaya hiyo Lazaro Twange ,amesema katika uchunguzi huu una kipengele cha hamasa,kwa maana ya kumpeleka ujumbe kwa wananchi kwa kupitia mbinu tofauti tofauti ikiwamo ya michezo
Kwanza wafahamu uchanguzi,lakini waelewe mafanikio na safari ya kuelekea kwenye uchaguzi wenyewe November 27 mwaka huu,
leo katika michezo tumewafahamisha umuhimu wa kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi jambo ambo linawapa sifa ya kuchagua Viongozi wa Serikali za mitaa ambao wanawapenda na kuwaletea maendeleao.
Lazaro amesema msisitiza wake mkubwa ni kuhamasisha wanatimiza wajibu wao wa kizalendo kama Wananchi kujiandikisha Kwa ajili ya Viongozi watakao watumikia , uandikishaji huo umeanza October 11 hadi October 20 mwaka huu
Mwisho