Na Mwandishi wetu
Geita
Kampuni Tanzu ya Umeme Tanesco (Etdco) inayojishughulisha na Ukarabati wa miundombinu ya Umeme katika maeneo mbalimbali imefanikiwa kujenga miundo mbinu na viunganishi vya migodi ya umeme nchini Tanzania.
Katika mahojiano na waandishi wa habari kwe Viwanja vya bombambili Mkoani Geita kwenye maonesho ya saba (7) ya Teknolojia ya madini Kaimu Mkurugenzi Huduma Za Ufundi wa kampuni ya Etdco mhandisi
Dismas Massawe amesema kuwa kampuni hiyo ni kampuni inayomilikiwa na Serikali yaani Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
kwa asilimia mia moja 100%.
Amesema mpaka sasa wamefanikiwa kujenga miundo mbinu kadhaa ya umeme,kujenga laini ya kilomita 100 kutoka Geita mpaka eneo la StamiGold ( Stamico ) na kuunganishia umeme.
Amesema, pia wamefanikiwa kujenga mradi mwingine wa kuunganishia umeme Mgodi wa GeitaGold mine (GGML) ,kujenga kilomita 58 kuunganisha umeme katika mgodi wa Kabanga nikel Ngara.
mhandisi
Dismas Massawe amesema kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa line kule Katavi,kuunganisha umeme katika maeneo ya migodi,pia wanaendelea na miradi mbalimbali maeneo ambayo sio ya madini kama miradi ya msongo wa kilovote 132 Tabora,miradi ya REA na miradi mingi ya Tanesco katika maeneo mbalimba nchini.
Amesema pia kwa sasa wako katika kutekeleza mradi wa Msongo wa kilovote 33,Kilomita 45 kutoka katika kituo cha Mpomvu mpaka Kasamwa.
Amesema hivyo ushiriki wao katika maonesho hayo ni kutoa elimu kwa sekta ya madini kuhusu kampuni yao hiyo,na kuitambulisha kampuni hiyo kuwa inafanya kazi ya ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya madini na uwezo wa kutekeleza miradi mikubwa na midogo katika kuunganisha umeme maeneo ya madini.
Amesema Lakini pia kuonyesha kazi zao wazifazo katika maeneo mbalimbali ili kuwezesha teknolojia ya madini,sekta ya madini iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Mhandisi Dismas Massawe ametoa wito kwa sekta binafsi na Serikali waweze kuitumia kampuni hiyo katika maeneo yao.
Mwisho