BAKWATA,wataka watoto kukaguliwa sehemu za siri wanapotoka shule.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto , wazazi wameshauriwa kuwa na tabia ya kuwakagua watoto wanapotoka shule.
Haya yamesemwa na Awazi Lema,Katibu wa Baraza kuu la Waislmu Tanzania (BAKWATA), Mkoa wa Kilimanjaro,wakati wa mazishi ya mke wa sheikh wa Wilaya Siha yaliyofanyika Kijijii cha Mlangoni Wilayani humo ,amesema wazazi wanapaswa kuwakagua watoto wanapotoka shule
Amesema hali ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto ni mbaya na hatua za kuthibiti hali hiyo lazima zichukuliwe ikiwamo kuwakagua wanapotoka shule Kila siku kwa kuwaogesha ili kama kuna kitu amefanyiwa liweze kugundulika mapema
Lema amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la matukio ya watoto kufanyiwa vitendo hivyo ikiwamo ubakaji na ulawiti jambo ambalo linaendelea kukua siku hadi siku ,hivyo hatutakiwa kufumbia macho hata kidogo ,inatakiwa kupambana kuokoa kizazi.
“Ni kweli kumekuwa na ongezeko kubwa la kesi za ulawiti na ubakaji dhidi ya watoto jambo ambalo linapaswa kushughulikia ili kumalizia
Sisi kama Baraza kuanzia ngazi ya mkoa , Wilaya,Kata,mpaka Msikiti tunawajibu wa kulisemea hili ,jambo kila tunapokutana ni agenda hiyo kupambana na ukatili,kina mama zetu tushirikiane pamoja na majukumu mlionayo tusisubiri mpaka mtoto ameharibika vibaya
Yasini Ibrahim Baadhi ya Waumini wameunga mkono wazazi kuwakagua na kuwaogesha watoto wao ,akisema ni jambo zuri,kwani kama mtoto amefanyiwa ukatili utagundua mapema na kuchukua hatua kuliko kukaa muda mrefu na kukuta mtoto alishaharibiwa
“Tutengeneze utaratibu wa kuwakagua na kuwachunguza mara kwa mara kwani wengi wao wanafanyiwa vitendo hivyo kutokana na uoga hawawezi kusema Kwa kuhofia vitisho walivyopewa”amesema Ibrahim
Sheikh wa mkoa huu Shaaba Mlewa,amewausia Waislmu na Wananchi kwa ujumla kutenda matendo mema na kuepuka yaleyaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu
Amesema hakika bora ya zawadi ni kumcha Mwenyezi Mungu,jiandaeni na kujiandaa ni kufanya ucha Mungu ,ucha Mungu ni kusamehe,ni uruma, kufanya ibada,kuacha fitina,kuacha umbea ,wezi,kutokudhulum ni ucha Mungu
Hizi ndiyo baadhi ya sifa nzuri ambazo mtu akizifanya akaacha mambo yote haya ,pale mahali kaburini pana kwenda kubadilika baada ya adhabu pale panakuwa sehemu ya furaha ,hivyo watu waendelee kufanya mambo mema hapa Duniani malipo watayaona.
Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka,mara baada ya kutoa pole ,aliwataka Waislmu na Wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi ili waweze na sifa ya kupiga kura na kuchagua kiongozi wa kuwaletea maendeleao, zoezi hilo limeanza wajitokeze kwa wingi
Mwisho