Mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro Saashisha Mafue ashiriki bonanza kuhamasisha watu kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi.
Mkuu wa Wilaya Hai mkoani Kilimanjaro Lazaro Twange amewataka Wananchi Wilayani humo kujitokeza kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi ili wawe na sifa ya kushiriki uchunguzi wa Serikali za mitaa November 27 mwaka huu.
Haya yamesemwa na Mkuu huyo wakati wa uzinduzi wa bonanza lilifanyika katika viwanja vya half Londan Bomang’ombe Wilayani humo, ambapo michezo mbali mbali ilifanyika ikiwamo mpira wa miguu
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo,amewaomba Wananchi kushiriki zoezi hilo la kujiandikisha lililoanza October 11 hadi October 20 mwaka huu.
Lazaro amesema uchunguzi huu una kipengele cha hamasa ,kwa maana ya kumpeleka ujumbe kwa wananchi kwa kupitia mbinu tofauti tofauti ni hii ni moja ya kipengele hicho
Kwanza wafahamu uchunguzi,lakini waelewe mafanikio na safari ya kuelekea kwenye uchaguzi wenyewe wa November 27 mwaka huu
Sasa pamoja na mambo mengine muhimu Wananchi wafahamu umuhimu wa kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi, ambalo limeanza rasmi October 11 mpaka October 20 mwaka huu
Kwa hiyo jamani msisitiza wangu mkubwa tuwafikishe tunatimiza wajibu wetu wa kizalendo kama Wananchi kwa ajili ya Viongozi watakao tutumikia.
Kwa hiyo lengo kukutana hapo ni hilo la kusisitiza kujiandikisha kwenye Daftari hilo ili uwe na sifa ya kupiga kura kuchagua kiongozi anakayeleta maendeleao
Mbunge wa Jimbo hilo Saashisha Mafue, amesema wapo hapo kuhamasisha na kukumbushana Wananchi wote wa Jimbo la Hai kujitokeza na kwenda kujiandikisha,amesema Mkuu wa Wilaya umuhimu wa kujiandikisha
Amesema sote tunafahamu kama unatafuta maendeleao yanaanzia katika Serikali za mitaa,kanuni yetu inatuambia Serikali za mitaa sauti ya Wananchi.
Hivyo tujitokeze kushiriki ,wale ambao mpo hapa tafadhali mkajiandikishe, tumuunge mkono Rais Samia Suluhuu Hassani zoezi liweze kufanikiwa
Hakikusheni mnapoenda kujiandikisha familia usiisahau pamoja na majirani, Viongozi wa kata endeleeni kuhamasiaha Wananchi
Mwisho .
Mwisho