Na Bahati Siha .
Wakazi wa Siha wa mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuuchukulia uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ukubwa wake na kuutendea haki kwa kuchagua viongozi watakaokuwa kiungo na sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili.
Haya yamesemwa Tumsifu Kweka mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa pia mjumbe mkutano mkuu wa mkoa,wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya SanyaJuu Wilayani humo ,
Kweka amesema uchaguzi huo ni muhimu na ni lazima ufanyike kwani viongozi watakaopatikana ni kiungo muhimu pia watakuwa na majukumu makubwa ya kujua hali na maisha ya wananchi wao kuanzia ngazi ya vijiji na mitaa kisha kuzipeleka shida hizo sehemu husika ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
“Sisi CCM hatujaja hapa kuomba kura kwasababu tu msimu wa kuomba kura umefika ila tumekuja hapa kuomba kura kwasababu tuna cha kuonyesha, tumefanya mengi na uwezo wa kuendelea kufanya hivyo tunao na ni kwaajili ya maendeleo ya wananchi na si vinginevyo hivyo niwaombe wananchi kwa umoja wenu naomba kura zenu siku uchaguzi mjitokeze kwa wingi mkipigie kura CCM,” amesema Kweka.
Amesema nyumba nzuri inajengwa na msingi uliobora, msingi wetu ndiyo huu sasa, November 27 mwaka huu kwenda kuchagua Viongozi wa CCM walipikika ambao wanaofaa kwenda kutuletea maendeleao
Kwa upande wake Mwenyekiti wa uwt kata hiyo ya SanyaJuu,Magrethi Kiungisu, amesema CCM kimetekeleza ilani yake kwa asilimia 90,kama kuna ambacho hakijatimizwa basi ni kidogo sana na wanaahidi uko wanapokwenda watamalizia sehemu iliyokuwa imeachwa
Hivyo kuomba Wananchi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi katika uchanguzi huu utakaofanyika November 27 mwaka, siku ya jumatano ambapo ni siku ya mapumziko.
Awali Diwani wa kata hiyo ya SanyaJuu Juma Jani ,amesema wakazi wa kata hiyo wana kila sababu ya kukipigia kura Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi huo kwani chama hicho kimefanya mambo mengi kwaajili ya maendeleao
“Tumefanya miradi msingi ikiwamo ujenzi wa Hospital ya Wilaya, Ujenzi wa barabara,miradi ya maji , umeme ,Kwa kweli ndani ya kata hii mambo yanefanywa mengi sana yaliyosalia ni machache ambayo yatakenda kumalizia,unajua hauwezi kufanya mambo yote Kwa wakati mmoja”amesema Jani.
Mwisho