Asema wananchi wasikubali kulaghaiwa na mtu yoyote na kuchagua chama kingine kwa sababu chama ambacho ndicho kitaweza kuwaletea maendeleo.
Hai ,Diwani wa kata ya Masama Kusini Sedrick Pangani , Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, amewaomba wananchi wa Kijijii cha mkombizi Wilayani hapa kuhakikisha wanakichangua chama cha mapinduzi (CCM)na wasikubali kudanganyika akidai kuwa hakuna chama kingine kinacho izidi CCM.
Pangani ametoa kauli hiyo Leo November 25,2024 wakati hitimisho ya kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kijijii cha Mkombizi Wilayani Hai mkoani hapa.
Amesema kuwa wananchi hao wasikubali kulaghaaiwa na mtu yoyote na kuchagua chama kingine kwa sababu chama ambacho kitaweza kuwaletea maendeleo ni ccm pekee.
“Ichagueni CCM, hakuna chama kingine ndugu zangu kwa sababu umichanganya rangi itakula kwenu na itakuwa umechezea kura hivyo niwaombe mkawapigie kura wagombea wote wa ccm ukizingatia Serikali ya awamu ya sita imeweza kuleta fedha nyingi kwa ajili ya utengenezaji wa miradi ya maendeleo.” Amesema Pangani
Pia Pangani amewataja wagombea hao Julius Malya mgombea Wenyekiti Kijiji cha mkombozi ,Abrahamu Michael kitongoji zarau ,Abutwalibi Juma,kitongoji korongoni ,Kadria Ulomi,kitongoji Mbololo,
“Ndugu zangu November 27 mwaka huu yaani kesho mkachague ccm ,hao wagombea niliowanadi wana kila sifa ya kuwa Viongozi ya kuwaletea maendeleao,ikiwamo kujenga chekechea ambapo watoto wa mkombozi wanatembea umbali mrefu kufuata masomo”Amesema Pangani
Awali mgombe huyo wa kijiji Julius Malya,akizungumza baada ya kupewa nafasi ya kuomba kura kwa wananchi wamehudhuria mkutano huo amesema kuwa wananchi hao wamchague katika uchaguzi huo ili aweze kuwatumikia wananchi wa mkombozi ikiwamo ujenzi wa shule mpya ya Sekondari inayojengea katika Kijijii hicho kupunguza umbali mrefu ya wanafunzi kufuata masomo
” Ndugu zangu naomba mniamini fomu nilichukua mwenyewe ya kugombea nafasi hii ili niweze kuwatumikia nawapenda sana natamani mkombozi yetu iweze kuwa mpya.” Amesema Julius
Kuna mambo mengi natarajia kufanya baada ya uchanguzi ikiwamo ujenzi wa barabara za kufungua ili ziweze kupitia vizuri,pia daraja lipo la kujenga yote haya baada ya uchanguzi yayafanyika naombeni kura ili tuweze kufanya haya niliyoyasema.
Mwisho .
Mwisho