Na Mwandishi wa A24tv.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda Novemba 21, 2024 amepongeza shirika la Mapadre la kazi ya Roho Mtakatifu(ALCP/OSS) kwa kuchangia katika huduma za kijamii ikiwemo elimu nchini.
Amesema hayo katika halfa ya Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo mwaka 1974 iliyofanyika katika makao makuu ya shirika Sabuko Sanya juu, Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro
Mkenda ametoa pongezi hizo kwa niaba ya serikali kwa kazi kubwa ambayo shirika linafanya nchini za kijamii na kuomba kanisa hilo liendelee kuliombea taifa kudumisha amani, umoja, mshikamano .
Amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na kanisa katika kuendesha gurudumu la maendeleo hapa nchini.
Mkenda amezungumzia mageuzi ya elimu na kueleza kuwa ifikapo 2027 elimu ya lazima Tanzania itakua miaka 10 badala ya miaka 7 na kusisitiza kuwa sheria na miundo mbinu ya shule inaandaliwa katika maeneo mbalimbali kukidhi utekelezaji wake.
” sisi ni kati ya nchi chache
tuluobaki na elimu ya lazima ya miaka Saba, mtoto anaanza shule akiwa na miaka sita anamaliza darasa la saba na miaka 13, halazimiki kuendelea sasa tumefanya mabadiliko” amesema Mkenda
Ameongeza kuwa kufuatia mageuzi baada ya miaka 6 ya elimu ya msingi itakuwa ni lazima kwenda sekondari mpaka kidato cha nne ambapo sekondari kutakuwa na mikondo miwili, mkondo jumla na elimu ya amali ambao ndani yake kuna Ufundi na Ufundi stadi.
Akizungumza Mkuu wa shirika hilo, Padre Charles Lyimo amesema shirika litaendelea kuwekeza katika husuma ya elimu kwa kuzingatia mwelekeo mpya ambao unalenga kukenga vijana wenye ujuzi.
” tunamshukuru Mungu kwa shirika kufikia Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 na kuliongoza shirika kutekeleza mipango mikubwa ya kuhusumia Jamii ikiwemo katika Elimu,” Padre Lyimo.
Mwisho .