Na Bahati Siha,
Diwani wa kata ya Evae’ny Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,Elinisaa Kileo,amewasihii Wananchi wa Kijijii cha Kishisha kutumia umeme kuwaletea maendeleao na kukuza uchumi wa eneo hilo
Haya yamesemwa na Diwani huyu wakati wa maombi maalumu ya Shukrani Kijijii cha Kashashi kitongoji cha Isuhun’y kupata umeme
Akizungumza na Wananchi waliokusayika katika tukio hilo,amewataka kutumia umeme huo kujiongezea kipato kwa kuwa wabunifu wa miradi na kuwa wajasiria mali.
“Ni kweli tumefanya ibada maalumu ya kushukuru umeme kuwaka ,kwani kwa miaka 4 nguzo za umeme zimepita hapa tulikuwa tunaziangalia, sasa mkutano huu ni kuto pongezi kwa wale wote walioshiriki hadi kufika hatua hiyo”amesema Elinisaa
Elinisaa amesema, kazi ya Serikali ni kuhakikisha inasogeza huduma karibu,kama ambavyo imewasha umeme leo katika eneo hili.
Amesema Sasa Wananchi jukumu lenu ni kutumia umeme huo kuwaletea maendeleao Kwa mtu mmoja mmoja na jamii nzima
Biashara mlizikuwa mnashindwa kuzifanya Kwa sababu ya kukosa umeme ,Sasa fungueni,fanyeni kazi fanyeni biashara mjiletee maendeleao
Aidha ametoa pongezi kwa meneja wa Tanesco mkoani hapo,kwa jitihada za kufanikisha umeme kufika eneo kwa kutoa transifoma, tunamshukuru Rais Samia Suluhuu Hassani kwani ndiyo anayetoa mafungu haya, Wananchi kwa miaka 4 walikuwa wakiziona nguzo zimepita katika Maeneo yao
Joseph Kileo,Anna Mmar wakazi wa eneo hilo, awali Wamesema Wamemshuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwasigezea huduma karibu.
“Ni kweli kushuru ni jambo muhimu sana,tulikuwa tunateseka kufuata huduma Maeneo mengine ikiwa ni pamoja na kuchaji simu,
Wakati mwingine unakutana na changamoto unapoenda kujichaji simu ,unaambiwa simu haijaaa inakubidi usubiri pia kuna kubadilishiwa betr ,inabidi kwenda kununua nyingine ,sasa umeme umefika tunashukuru.
Mwisho
Mwisho