Na Bahati Hai,
Katika kusherekea Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhamedi (SAW), Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), mkoani Kilimanjaro limekusudia kupanda miti 5000 ambayo wanauwezo wa kuimudu kuitunza ,kwa Wilaya zote mkoani hapa,ikiwa ni ibada pia kumuunga mkono Rais Samia Suluhuu Hassani katika jitihada za kutunza mazingira
Haya yamesemwa leo na sheikh wa mkoa wa huo Mlewa Shaabani wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti kimkoa ikiwa ni Maazidhimisho ya Maulidi,uliofanyika katika Zahanati ya Bomang’ombe Wilayani Hai mkoani hapa.
Ambapo pia ametoa magizo kwa masheikh wa Wilaya zote mkoani hapa kusimamia na kuhakikisha miti iliyopandwa inakuwaa na kuachana na kasumba iliyozoeleka ya kupanda miti na kuitelekeza
Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo ,amewataka masheikh hao pia na taasisi nyingine zinazopanda miti kusimamia miti yatakayopanda inakuwe na kufikia malengo ya liyokusudiwa ya Tanzania kuwa ya kijani
Mlewa amesema amelazika kusema hivyo kwa kuwa kumakuwa na kasumba iliyozoeleka ya watu kupanda miti bila kugeuka nyuma kuangalia kama miti hiyo imekuwa jambo ambalo sio zuri
Amesema watu hao wakishapanda na kupiga picha ili kuonekana wamepanda wanaondoka na hawarudi kuja kuihudumia tena na hatimaye miti hiyo ufa,hivyo kushinda kufikia malengo yaliyokusudiwa ya Tanzania kijani
“Ni kweli kumezuka kasumba ya watu na Baadhi ya taasisi wanapoadhimisha jambo flani ukimbilia kupanda miti na kupiga picha nyingine na kuondoka bila kujua nani ataisimamia miti hiyo itunzwa na kukua matokeo yake miti hiyo ufa
Ndiyo maana sisi tumeelekeza ipandwa miti michache kwa sababu hatutaki kupanda miti alafu tujeituta imekufa hatutaki jambo hilo litokee,ili na wengine waige kutunza miti waliyopanda
Diwani wa kata ya Bomang’ombe Wilayani humo,Evod Njau, ameishukuru BAKWATA,kwa kuona umuhimu wa kuzindua zoea la upandaji miti katika kata yake,kwa namna ya kipekee ameshukuru sana.
Na naahidi kwa namna ya kipekee kujilinda miti wanaahidi hiyo,kwa sababu wapo Viongozi wote wa Serikali,tuta weka ulinzi ili angalau leo na kesho waendelee kuona ikiendelea kumea vizuri
Kwa upande wake Afisa mazingira Wilayani humo Haveneti Urasa ,ameahidi kutupia jicho miti hiyo na kuhakikisha inakuwa ili kufikia lengo la upandaji wa miti na kumuunga mkono Rais Samia Suluhuu Hassani
Miti ni muhimu,miti ni uhai, sheikh wa mkoa kama alivyosema upandaji wa miti ni ibada kwa hiyo ni jambo jema,
Mwisho