Na Bahati Hai .
Hai,Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lazaro Twange amewataka Wananchi Wilayani humo kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa kwenye kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura kuanzia December 11 mwaka huu ili wawe na sifa ya kupiga kura
Haya yamesemwa na Mkuu huyo wakati wa maadhimisho miaka 63 ya uhuru wa Tanzania yaliyofanyika katika ukumbi wa halmshauri na kuhudhuria na Wananchi, Madiwani,Wakuu wa idara pamoja na Wadau wengine wa maendeleao,ambapo ilikwenda sambamba na uchangiaji damu.
Akizungumza mara baada ya kupata frusa hiyo ,amewataka Wananchi Wilayani humo kujitokeza kwa wingi ili kuweza kutimiza wajibu huo wakijiandisha ili kuwa na sifa ya kuwa mpiga kura na kuchagua kiongozi wa kuleta maendeleao,
“Kuanzia December 11 hapa Wilayani kwetu na sehemu nyingine kwenye mkoa wetu wa Kilimanjaro zoezi la kujiandikisha na kuboresha taarifa zetu kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura litaanza naomba mjitokeze ndugu zangu”amesema Lazaro
Kila mmoja kwamba nafasi yake ,kama tukivyofanya kwenye uchanguzi uliopita wa Serikali za mitaa , Viongozi wa Dini na wengine tunaomba habari hizi mtufikishie kwa Wananchi wajitokeze wakajiandikisha.
Amesema kujiandikisha unaweka uhalali wa kupiga kura mwaka kesho,anaweza akatokea mgombea unayempenda,tukajazana sana uwanjani kwenye mikutano yao na tukawa na hamu wagombea wetu washinde ,tunabaki kuishia watazamaji kama hatutakuwa tumejiandikisha
Naomba sana tukajiandikishe ili tuwe na sifa ya kupiga kura ,atakayetokea mwaka kesho ni sehemu ya sisi kuamua yatokee kama yatakavyotokea
Akizungumza kuhusu swala la miaka 63 ya uhuru , amesema Serikali imefanya mengi ,Nirudi kwenye mada hii ya miaka 63 ya uhuru ,Mimi nitaongelea vitu vidogo vidogo vile vinavyo onekana onekana, mambo mengine ameshasema Mkungenzi mtendaji wa halmshauri
Lazaro amesema kwamba amekuwa akikutana na Baadhi ya watu wanalalamika ,wanasema miaka sijui 60 ya uhuru hakuna kilichofanyika, uwa nawashangaa sana
Kwa mfano mtu anajirekodi alafu clip anairusha kwenye mitandao ya kijamii akilalalamika kwamba hakuna kilichofanyika,
Mtu kama huyo nashindwa kumuelewa ,hicho kifaa alichojirekodia na kurusha kwenye mitandao hadi sisi tukakisoma ni matokeo ya miaka 63 ya uhuru
Hivi mwaka 61 kurudi nyuma uko ,kulikuwa na jambo kama hili,ni kwamba hapa kuwa na vitu kama hivi,mambo mengine yanafanyika nadhani wapo wazee ni mashuhuda wa hichei ninachoongea
Kwa hiyo nachotaka kusema nivizuri tukawa na maneno ya akiba ,sio vibaya kueleza yale ambayo unafikiria bado hayajatoka ili yatokee
Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Edmund Rutaraka, amesema kuna mabadiliko makubwa sana ndani ya Wilaya hiyo toka kupata uhuru ,mambo mengi sana yamefanyika,umeme upo wa kutosha,maji yapo , barabara,sisi tulizaliwa zamani tunaona tofauti kubwa ,watu tulikuwa tunasoma usiku kwa kutumia kibatari ,tunaenda shuleni bila viatu lakini sasa tupo Kuna tofauti kubwa
Awali katika taarifa yake Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Dionis Myinga, amesema toka Rais Samia Suluhuu Hassani kuingia madarakani halmshauri imepata zaidi ya sh,45 billion kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleao
Amesema miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya Madrasa shule za msingi, Sekondari na vyumba vya Madrasa ya awali , matundu ya vyoo, pia ujenzi wa barabara, vituo vya Afya,Maji na mengineyo mengi,tunnampongeza Rais kwa fedha hizo kwa ajili ya maendeleao ya Wananchi wa Hai
Mwisho