Na Bahati .
Ofisi ya meneja wa Wakala wa barabara mkoani Kilimanjaro (TAN ROADS), imeingia mkataba na Mkandarasi aitwae Kings Builders LTD ,kutoka jijini Dar es Salaam ya ujenzi wa madaraja 7 pamoja na kunyanyua tuta la barabara kilo mita 1.5 katika maeneo yenye urefu wa mita 500 na mita 1,725 eneo la kwa wasomali lilipo Wilayani Hai ,yenye thamani ya sh,5.8 billion
Haya yamo katika taarifa yake aliyo wasilisha mbele ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdini Bab na Engineer Benitho Mdzove kaimu Meneja wa Tan road mkoani hapa wakati wa makabidhiano wa mkataba huo wa kazi , uliofanyika kata ya Kia Wilayani humo.
“Leo tumekutana hapa ili kushuudia hafla ya kukabidhi Mkandarasi eneo la kazi kwa mkataba wa ujenzi wa madaraja 7 pamoja na kunyanyua tuta la barabara kino cha mita 1.5 katika maeneo yenye urefu wa mita 500 na mita 1,725 eneo la kwa wasomali lilipo Wilayani Hai “amesema Benitho
Katika taarifa yake hiyo amesema Mkoa wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa ambayo iliathiriwa na mvua za Elnino zilizonyesha Nchini kuanzia mwishoni mwa mwaka jana hadi mwanzoni mwa mwaka huu
Serikali imepata fedha hizo kutoka Bank ya Dunia kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya Daraja katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua ya El nino kwa mkoa wa Kilimanjaro.
Amesema mvua hizo zilileta athari mbali mbali katika miundombinu ya barabara.katika mtandao wa barabara za mkoa wa Kilimanjaro, barabara za mkombozi (KLM)/Tanga Border)Himo njia panda ni moja ya barabara zilizoathirika na mvua hizo
Kutokana na athari hizo Wakala wa barabara iliweka mpango huo wa kuboresha eneo hili la kwa wasomali ,ambapo Mradi wa ujenzi wa madara 7 pamoja kunyanyua tuta la barabara kino cha mita 1.5 katika maeneo yenye urefu wa mita I,725 ni moja ya miradi ya dharura inayotekelezwa Nchini ili kuboresha /kurekebisha miundombinu iliyoathiriwa na mvua hizo za El nino
Kwa upande wake ,Mkuu wa Wilaya hiyo lazaro Twange, amesema kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya hiyo,anatoa Shukrani Kwa Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kuwapa fedha hizo hizo Kwa ajili ya kuboresha miundombinu ,Tanzania ni kubwa sana lakini kwa njinsi Rais anawapenda watu wa Hai anawajali amefanya kuleta fedha hizo,tupo moyani mwake , tunamshukuru
Aidha Diwani wa kata hiyo Tehera Mollel, amesema eneo hilo linalowekwe madaraja limekuwa kero kubwa kipindi cha masika, maji yamekuwa yakifurika na kuharibu mashamba ya wakulima na kupitia juu ya barabara ya lami mara kwa mara na kusababisha baadhi ya magari kuzobwa na maji, tunashukuru kwa ukarabati huo
Naye Mkuu wa mkoa huo Nurdini Babu,amemtaka Mkandarasi aliyekabidhiwa kazi hiyo,Mradi unaanza mara moja na Mradi huo unatarajia kukamilika September 25 mwakani kabla ya kupiga kura kuchagua Rais,Wabunge pamoja na Madiwani
“Ni kweli Mradi huo naomba Mkandarasi kuzingatia makubaliano ya mkataba na thamani ya fedha iwezekuonekana , Mkandarasi umesikia”amesema Nurdini
Mwisho