katika siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili (TAPO), Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro ya toa msaada kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kata ya Nasai Wilayani humo
Siha,Jamii imeshauriwa kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu,ili kukabiliana na wimbi la watoto kuzuzura mtaani hivyo ambapo baadhi yao ujikuta wakijiingiza kwenye makundi ya kiharifu hali ambayo inahatarisha usalama wao.
Rai hiyo imetolewa Rhoda Mshomi ambaye ni Mwenyekiti wa (TAPO), Wilayani ya Siha kinachojiusisha na ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake ,wakati wa kukabidhi misaada mbali mbali ikiwamo Michele na sabuni katika kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo kata ya Nasai Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro katika siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili
Akizungumza mara baada ya kutoa misaada hiyo,ameomba jamii kuhakikisha kwamba inasaidia watoto hao ili wawezo kukua katika makuzi mazuri yenye tabia njema.
Rhoda ,mesema kwa sasa kuna wimbi kubwa la watoto wa mitaani kutoka na Wazazi na walezi kuwatelekeza kutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na ugumu wa maisha,na kusababisha baadhi yao kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na wengine wakifanyiwa vitendo vya ukatili
“Sisi kama jamii tunalo jukumu kubwa la kuhakikisha hawa watoto wanasaidika uko walipo ili tuweze kuokoa kizazi kijacho
Tutafanya hivyo ili na wao wasione kwamba wamesahaulika ,hawa watoto ni wetu ,tuwasaidie,na kwamba uyatima hawakuomba wamejikuta tuu wakiwa hivyo hivyo tuwasaidie
Pia sambamba na hilo amewapo somo la kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ,wanapoona viashiria za kufanyiwa vitendo vya ukatili ikiwamo kushikwa shikwa sehemu za miili yao ikiwamo matiti au makalio watoe taarifa kwa mtu wa karibu yao wanayemuamini akiwamo mwalimu na mzazi ili wawezo kusaidia wasikaa kimya
Sambamba na hilo amewataka Wazazi na walezi kuwajengee uwezo watoto wao namna ya mapambana dhidi ya ukatili katika jamii,mambo ya kuzingatia unapozungumza naye ni pamoja na kumpa mbinu za kujilinda
Ukimpa elimu hiyo mtoto unamuongezea usalama wake ,wakati mwingine wao hawaelewi ,wanaweza kudanganywa, haya yote ni katika jitihada za kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama na kuwa na kizazi kizuri na chenye nizamu
Kwa upande wake Peter Msaka Afisa maendeleao ya jamii Wilayani humo,amewataka wazazi kuwa na lugha nzuri mbele ya watoto, baadhi ya Wazazi wamekuwa chanzo cha watoto kuharibiwa ,
Hatma ya maisha ya mtoto wako inategemea namna gani , wazazi na walezi wanavyishi,kama mnatamka maneno machafu mbele yao na wao wanakuwa na kuiga tabia hiyo,hivyo tunapokuwa mbele ya watoto wetu tujitahidi kuongea maneno mazuri hata kama kuna mkwaruzwana
Akishukuru kwa msaada hiyo,Mkuu wa kituo hicho, Ester Lema,amesema baada ya kuona watoto ni wengi wapo mtaani hawana msaada aliamua kuanzisha kituo hicho ili kuwasaidia kwa kushirikiana na Wadau.
Tunashukuru msaada hii ambayo tumeletewa leo kwa ajili ya kuwasaidia watoto wetu ,hii ni zawadi kubwa ,tunaomba Wadau wengine waendelee kutuunga mkono
Mwisho