Na Geofrey Stephen Arusha.
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Yas imepeleka huduma za mawasiliano katika eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro na Simanjiro mkoani Manyara ili kuwezesha wananchi wa pembezoni kupata mawasiliano kwa kasi ya 4G na 5G Kanda ya Kaskazini.
Akiongea na wanahabarimwa Jijini Arusha , Ofisa Mkuu wa Biashara kutoka YAS, Isack Nchunda juu ya mabadiliko ya chapa ya kampuni ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Kanda ya Kaskazini amesema upelekeaji wa mawasiliano hayo haswa maeneo ya Loliondo na Simanjiro ni kuboresha huduma bora za mawasiliano
“Tumefika maeneo yenye changamoto ya mawasiliano kwa kasi ya 4G na 5G lakini pia huduma zetu za tigo pesa sasa zinajulikana kwa Mixx by Yas ikiwemo kampeni yetu ya magift ya kigift ambayo wateja wetu wanashinda zawadi mbalimbali za fedha taslim pamoja na gari ”
Amesisitiza kwa kanda ya Kaskazini mshindi wa kwanza kupata gari, Ibrahim Idd amepatikana na wiki ijayo atakabidhiwa gari lake aina ya KIA Selstos mkoani Manyara.
Awali Kaimu Mkurugenzi kanda ya Kaskazini, Daniel Mainoya alisema Yas Kanda ya Kaskazini imejipambanua karika mageyzinya kidigitali Tanzania kutoa huduma bora kwa wateja wake zitakazoenda sambamba na mabadiliko hayo makubwa ya chapa ya Yas.
Alisema Yas Katika kipindi cha Miaka miwili mfululizo imetunukiwa tuzo ya kimataifa kama mtandao wenye kasi zaidi nchini Tanzania wenye minara maeneo mengi zaidi yenye kusoma 4G na 5G.
SG “Kwa sasa tunateknolojia zote tano 26,3G,4G na 5G ambapo 5G ndio Teknolojia ya mwisho yenye kasi kubwa kwa sasa ,ukienda Moshi utakutana na 5G,Ukienda Babati utakutana na 5G ,pia tumetanua wigo maeneo ambayo hatukuwepo ,mfano Longido, Loliondo, Lengijave, Simanjiro na maeneo mengi ya kanda ya Kaskazini utakuta Yas ipo kwa kasi zaidi”Alisema.
Mwisho .