Na Bahati Hai,Mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro Saashisha Mafuwe, amesema kumeibuka vitendo vibaya vilivyokithiri katika Wilaya hiyo ikiwamo ukatili wa kijinsia,wezi, uhalifu pamoja na ulevi uliokithiri kwa vijana hivyo kupunguza nguvu kazi ya Taifa
Haya yamesemwa na Mbunge huyo katika serehe za Maulidi ya kuzaliwa Mtume Muhamedi (SAW) yaliyofanyika katika Msikiti mdogo mtaa wa uzunguni Bomang’ombe Wilayani humo kimkoa ambapo Wilaya zote za mkoa huu na nje ya mkoa ziliweza kuhudhuria pamoja na Viongozi mbalibali wakiwamo wa Serikali.
Akizungumza kwenye sherehe hizo mara baada ya kupata nafasi , mgeni rasmi sheikh wa mkoa wa Arusha shaabani Juma,ameomba Viongozi wa Dini kwa umoja wao kusaidiwa kuwekeza nguvu katika kukemea mambo haya ili kizazi kuweze kubaki salama
“Ni kweli naombeni jambo moja masheikh wangu mnafanya kazi ngumu ,kumeibuka sasa hivi utatili wa kijinsia ikiwamo ubakaji na ulawiti uliokithiri,ulevi uliokithiri,wizi na uhalifu uliokithiri ,sasa tusaidiane katika ili kulenda nguvu kazi ya Taifa ili tupate maendeleao tulinde kizazi “amesema Saashisha.
Amesema,kwa masikitiko niseme kwamba masheikh mpo hapa ,mtusaidie hawa wenye shida ninao sema hawapo hapa ,mtusaidie kufikisha salamu kwa masikitiko niliyonayo
Lakini sio Mimi tuu alikuja Makamu wa Rais hapa philip Mpango,akatukemea kuhusu ulevi uliokithiri,Waziri mkuu Kasimu Majaliwa wakati wa uzinduzi wa mbio za Mwenge Kitaifa mkoani hapa,tulikuwa wote,alikemea jambo hilo,halitupi heshima sisi watu wa kasikazini
Saashisha kitolea mfano ,amesema kuna siku alifanya ziara kwenye shule moja kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni, wakazi wa eneo hilo wakamueleza changamoto ni vijana kufanya kazi siku moja ,kesho yake hawafiki ,kwani wamekula wameshiba kupitiliza hivyo kazi hawaendelei tena hii sio sawa
Amesema hizi jitihada anazofanya Rais Samia Suluhuu Hassani,zinaweza kufifishwa kwa kukosa watu wa kunufaika na jitihada hizo
Masheikh nisaidieni jambo hili ,nisaidieni kusema na watu wa Mungu ili turudi nyuma na tuendelee kuishi kwa mafunzo tuliopewa na Mtume Muhamedi (SAW)
Lakini pia Wazazi mliopo hapa ,semeni na watoto wenu ,tusepo sema sisi,watakuja watu wa nje watasema nao,tuzungumze kuhusu maadili na kuwajenga wenye tabia njema.
Maustazi mliopo hapa,mtusaidie kuwalea watoto wetu uko Madrasa endeleeni ,nawaomba sana mfanye kazi hii kwa bidii ilikujenga chenye kumjua Mungu, kizazi ambacho kinamcha Mungu na mwisho wa siku sote tuweze kukutana kule Ahera
Hivi karibuni Mchungaji Thomas Kudalisamu wa Doyasisi ya kaskazini Jimbo la Hai usharika wa Ng’uni,akiwa kwenye sherehe fupi kwenye kituo cha kulelea watoto yatima Lukani Children center, alisema kuna uuzwaji wa pombe karibu kila nyumba katika Kijijii cha Ng’uni
Lakini serikali ipo hakuna wa kuthibiti hili,kwa sababu hiyo vijana wengi wadogo sasa wanajikuta wanakosa maadili nguvu kazi ya Taifa inapungua Kwa sababu muda wote vijana wamelewa,ili kuthibiti hili ni lazima ifike mahali Kanisa Sarikali na wazazi kuwa na ushirikiano wa kuhakikisha linadhibiwa jambo hili mapema
“Ni kweli bila ushirikiano wa Viongozi Dini, Serikali pamoja na Jamii hakuna kitu kitawezekana bila ushirikiano,pia na Wabunge waangalie hili jambo “amesema Thomas
Katibu wa BAKWATA mkoani hapa Awazi Lema, amesema tayari BAKWATA wanakitengo cha kutoa elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia na kinafanya kazi kwa kutoa elimu sehemu mbali mbali ikiwamo kwenye shule za msingi na Sekondari
Na kwamba wataendelea kutoa elimu dhidi ya ukatili ikiwa ni ubakaji na ulawiti ili jamii ya Kitanzani ibaki salama kwa kushirikiana na Serikali
Mwisho