Na Bahati Siha .
Abiria wanaosafiri na Daladala za SanyaJuu Bomang’ombe na Moshi mjini pamoja na SanyaJuu West Kilimanjaro,Wametakiwa kabla ya kupanda kwenye magari hayo wahakikishe wanangalie ubavuni wa magari kumeandikwa nauli halaliĀ wanazopaswa kulipa ili kuepuka usumbufu wakati wa kulipa nauli
Haya yamesemwa Paulo Nyello Ofisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafirishaji aridhini( latra) mkoa wa Kilimanjaro, baada ya kuwepo malalamiko kwa Abiria kwamba magari hayo yakiwamo Noah na haice yamekuwa yakipandisha nauli kiholela na kusababisha usumbufu kwa Abiria hao.
Akizungumza na waandishi wa habari,kuhusu jambo hilo amewataka Abiria wote kabla ya kupanda kwanza waangalie upande wa ubavuni kumechorwa nauli ya kila kituo anachoshukia Abiria na kiwango anachotakiwa kulipa
“Ni kweli kabla ya kupanda jiridhishe kwanza angalia ubavuni nauli zimeandikwa kila kituo na pia namba za latra kupiga Bure kama kuna usumbufu umetokea hivyo Abiria wazingatie hilo nazani itasaidia kudhibiti tabia “amesema Paulo
Paulo amesema zoezi hilo la kuandika namba ubavuni baada ya malalamiko mengine kutoka kwa Abiria kuhusu nauli kupandishwa kiholela ,tuliona ni busara kila gari kuandika nauli ubavuni ili kuweza kumsaidia Abiria
Sasa pamoja na kuweka utaratibu huo,bado tunapokea malalamiko,ndiyo sababu imenilazimu kusema kuwa kabla Abiria hajapanda kwenye magari hayo kwanza aangalie ubavuni mwa magari hayo nauli zote za vituo vimechorwa amesisitiza
Sisi wakituona barabarani wanapeana taarifa kwamba larta wapo na kuanza kutoza nauli halali, hivyo sio rahisi kuwabaini,labda kwa kuwa kustukiza ndiyo sababu ya kuomba wafanye hivyo ili kuepuka usumbufu huo.
Awali baadhi ya abiria akiwamo Samweli Mbise mkazi wa Ngarenairobi, amesema wamekuwa wakitozwa nauli ya shilingi 2000 hadi 3000 ,kutoka Sanya juu hadi Ngarenairobi west Kilimanjaro,jambo ambalo sio sahihi
Wakati mwingine ukihoji utingo wa gari anakutishia kukushusha au anakwambia usipande gari yake na wakati mwingine Abiria mwenzeko hawakusaidie wakati unalalamika wao wanaendelea kutoa nauli ,hapo unajikuta umejipata umelipo nauli isiyo sahihi na kama haukubeba hela ya ziada ndiyo changamoto kabisa
Pia ukiwa na mzugo ambao ni mdogo unaambiwa ulipie shilingi 1000 na kuendelea kwa kweli hii Abiria wananyanyasika utasema hatuna Viongozi
Anna Kileo mkazi wa SanyaJuu, anesema nauli kutoka Bomang’ombe Wilayani Hai hadi SanyaJuu kwa kweli inashindwa kufahamu bei halisi ,mara unalipa shilingi 1500 mara unalipa shilingi 2000 ,3000 wakati mwingine 1000 ,ili ni tatizo
Mwisho