Na Mwanfishi wetu Siha,
Watoto wa tatu wa familia mmoja wamefariki Dunia Kijijii cha Ngaratati kata ya Makiwaru Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,wakati wakioga kwenye Lambo lilijengwa na Serikali kwa ajili ya mifugo kupata maji
Diwani wa kata hiyo Ezekiel Lukumai Akizungumza na waandishi wa habari amesema,Tukio hilo limetokea Junuary 2 mwaka huu, wakati watoto hao walipoenda katika eneo hilo kwa lengo la kufua nguo na kuoga
“Ni kweli watoto hao wamefariki Dunia kwenye lambo hilo wakati wakiogelea mmoja ana miaka 9 darasa la nne shule ya msingi Ngaratati na hao wawili miaka 6 wapo chekechea , kati ya hao watatu wawili ni wa Mwenyekiti wa kitongoji cha Lambo na mmoja ni wadungu yake uzuni mkubwa sana kupoteza watoto hao “amesema Ezekiel
Akielezea kwa undani kuhusu tukio hilo ,amesema siku ya tukio watoto hao ,ambao ni wakike ,walikuwa na baba yao mzazi hapo nyumbani, mzazi huyo aliingia ndani kwa lengo la kujipumzisha
Amesema baada ya watoto hao kuona baba yao ameingia ndani , wao kuondoka nyumbani na kwenda kwenye Lambo hilo ambalo halipo mbali na nyumba wanaoishi,kuoga na kufua nguo , nadhani maji yaliwazidi na kufikwa na umauti wakati wakiogelea
Ezekiel amesema walipata taarifa hizo kutoka kwa watoto wengine walifika katika eneo hilo,na ndiyo zikapigwa kilele za kuomba msaada Wananchi walifika ,ambapo walikuta karai na nguo zilikuwa zimefuliwa pembeni
Pia watoto hao wakiwa wamefariki wameelea juu ya maji na jeshi la Polisi walifika na kuchukua maiti ambapo zimehifhiwa hospital ya Kibongoto
Wito wangu kwamba kwa Wananchi wasiruhusu watoto kupeleka mifugo katika eneo hilo ,watu wazima ndiyo wafanye jukumu hilo, kuepuka tatizo kama hili lisijitokeze tena
“Ni kweli tusiruhusu watoto kupeleka mifugo eneo hilo kwani wamekuwa wakionekana kuogelea na pia pawekwe uzio ili kuwa na ulinzi wa kutosha”amesema Ezekiel
Hili lambo lilikuwa na uzio lilipojengwa ,lakini watu walifanya uharibifu,naomba Wananchi waendelee kulilinda,kwa sasa tunaomba Kijijii waweke uzio hata wa kupanda katani na Serikali nayo iangalie namna ya kusaidiwa kuweka uzio ili kuweza na usalama
Julius Mollel,mmjo ya Wakazi wa eneo hilo, amesema upungufu wa maji kwenye mabomba unachangia baadhi ya watu kwenda kufua nguo kwenye lambo hilo,hata hawa inaweza kuwa na sababu
“Maji kwa wiki yana kuja mara moja au mbili kwa wiki, ili ni tatizo katika eneo hili hivyo kusababisha watu kwenda kufua nguo kwenye eneo hilo “amesema Mollel
Mwenyekiti wa Kijijii hicho Nurueli Kivuyo, amekiri kutokae kwa jambo hilo na kwamba watoto hao walienda kufua nguo na kuingia kuoga na wengine huwa wanaogelea sijui nini kiliwakuta na kukutwa sehemu mmoja wakiwa wamefariki
Kingine kuna uhaba wa maji kwenye mabomba kitu kinachosababisha kwenda kufua nguo kwenye eneo hilo
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Simon Maigwa amesema,kwema yupo nje ya ofisi na kwamba atafuatilia hapo ofisini kama wanataarifa
Mwisho