Na mwandishinwa A24tv .
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 25.01.2025 imetoa elimu kinga dhidi ya madhara ya dawa za kulevya kwa wananchi waliohudhuria Maadhimisho ya ufunguzi wa Wiki ya Sheria mkoani Arusha yanayoendelea kuhadhimishwa katika viwanja vya TBA Kaloleni.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria kwa Mwaka 2025 ni; *_”Tanzania ya 2050: Nafasi ya Taasisi Zinazosimamia Haki Madai Katika Kufikia Malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo”._
DCEA kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kaskazini kwa pamoja walikuwa na banda maalum la kutolea elimu ambapo Mamlaka ilichukua fursa ya maadhimisho hayo ili kuwaasa wakazi wa Mkoa wa Arusha kuachana na matumizi pamoja na biashara haramu ya dawa za kulevya lakini pia walifahamishwa kuhusu sheria kali dhidi ya wahalifu wa dawa za kulevya ambapo adhabu yake hadi kifungo cha maisha jela na mali za mtuhumiwa kutaifishwa na kuwa mali ya umma.
*_Mwisho, Wananchi waliohudhuria ufunguzi wa maadhimisho hayo waliombwa kushirikiana na Mamlaka katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini kwa kuwaumbua na kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga simu ya bure 119._*
*_MWISHO_*