Na Geofrey Stephen Arusha .
Bilioni 5.4 zimetumika kuboresha huduma za afya katika hospital ya Mkoa wa Arusha Mount Meru katika kununua vifaa mbali mbali vya matumizi ya kufanyia wagonjwa sit scan pamoja na mashine za kufanyia operesheni kwa njia ya kisasa .
Fedha hizo ambazo zimetolewa na wadau wa maendeleo katika mkoa wa Arusha zimelenga kuboresha sekta ya Afya na kupunguza makali ya ya garama za matibabu kwa wananchi wa hali ya nchini wasio jiweza .
Katika hatua nyingine Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru inatarajia Kuzindua Huduma mpya za afya kwa wananchi wake ikiwa ni Pamoja na Upasuaji kwa njia ya Matundu, Utoaji huduma ya dawa za Kansa na Uzalishaji wa hewa tiba itakayosaidia kuokoa maisha ya wananchi.
Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa huo, Dkt Alex Ernest alipokuwa akitoa taarifa ya utekeleza katika robo ya pili ya mwaka wa serikali katika hospitali ya Mount Meru.
Dkt. Alex ameeleza kuwa huduma mpya ya upasuaji kwa njia ya matundu inatarajiwa kuanza kazi mwezi wa kumi mwaka 2025 ambapo itasaidia kuokoa gharama na muda wa mgonjwa kukaa hospitalini, kuongeza ufanisi wa kazi kwa watoa huduma, Pamoja na kupunguza madhara na kubakia na kovu dogo zaidi baada ya kufanyiwa upasuaji.
“Huduma hii ya upasuaji kwa njia ya matundu itaanza kutolewa mwezi wa kumi mwaka huu 2025 na itasaidia kuokoa gharama na muda wa mwananchi kukaa hospitalini, itaongeza ufanisi, na kupunguza madhara ya kubakia na kovu kubwa baada ya upasuaji”. Amesema Dkt. Alex Ernest Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mount Meru.
Aidha Ameeleza kuwa Wadau Mbalimbali kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wamejenga jengo la tiba Kemia Ambalo litaanza kutoa huduma ya Matibabu ya Kansa kuanzia mwezi wa tano mwaka 2025, kwa Wananchi wa Mkoa wa Arusha na Mikoa Jirani ambapo huduma hiyo itasaidia kupata dawa na kuokoa gharama za kusafiri kwenda kutafuta huduma mbali,.
Dkt. Alex amebainisha kuwa jengo hilo limejengwa na wadau wa maendeleo kutokana na faida ambazo wamezipata baada ya Mh. Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassani Kufungua Milango ya Utalii kupitia Filamu ya “The Royal Tour” ambayo imeleta matokeo makubwa kwa wananchi.
Pamoja na hayo, huduma yingine mpya zinazotarajiwa kuanza kutolewa kwa wananchi ni pamoja na upatikanaji wa majibu ya sampuli za damu baada ya kukamilika kwa jengo la Damu salama, kuanza kwa huduma ya nyumbani.