Na Bahati Siha,
Kaimu Mkurungenzi mkuu wakala wa maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA)Wolta Kirita, amesema Ruwasa imeingia kwenye makubaliano na chuo cha ufundi kilichopo mkoani Arusha kubuni mitaa kabla ya malipo(prepaid Weter)
Ambapo lengo kufunga mita hizo ili kuondoa malalamiko ya Wananchi ya madai ya kubambikiwa bili , kukabiliana na changamoto ya malimbikizo ya madeni na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Serikali.
Haya yamesemwa February 8 ,2025 na Kaimu Mkungenzi huyo katika ziara ya kutembea Bodi ya maji ya Lawate fuka iliyopo Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kuangalia skimu inavyofanya kazi,ambapo pia ameambatana na wajumbe wa bodi ya wakungenzi Ruwasa
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika eneo la Bodi ya maji Lawate fuka, amesema lengo la ni kutembea skimu hiyo pia namna bora ya kufunga mita hizo ni mikakati wa kukabiliana na malimbikizo ya madeni na.
“Ni kweli lengo kufunga mita hizo ni mikakati wa kukabiliana na changamoto ya malimbikizo ya madeni ya maji,pia kuongeza ufanisi katika ukusanyaji mapato ya Serikali na upotevu wa maji”amesema Wolta.
Wolta amesema makubaliano waliyoingia na chuo hiko kutengeneza mita hizo ,kulikuwa na hatua ya awali,kwa maana ya pailoti hatua hiyo imeshapita ,ilikuwa hatua ya majaribio na zile mita zimeshatengenezwa na kufungwa maeneo mbali mbali ikiwamo hapa Bodi hii ya Lawate fuka
Amesema wajumbe wa Bodi wamekuja kuangalia mahali zinapotengenezwa na sehemu zilipofungwa ,kama mlivyosikia Viongozi wa chombo hiki baada ya kufunga mita hizo yale maeneo yenye shida kubwa ya madeni , madeni yamepungua
Kwa hiyo lengo la taasisi hii ya Ruwasa ni kuja sasa kuingia makubaliano na chuo hicho kuzalisha mita nyingi zaidi ili zifungwa zaidi maeneo mbali mbali kwenye miradi vijijini.
Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka, ameshukuru Bodi pamoja na menejement ya Ruwasa kwa kuchagua Siha kuwa moja ya wilaya ya kufanya majaribio
Na kutokana na majaribio hayo ,wamewaza kujifunza nini ambacho kinaendelea , lakini kwa sababu mmefika hapa mtajionea wenyewe hata kama kuna changamoto mdogo mdogo itakuwa wakati mzuri wakujifunza hapa na kwenda kuzifanyia kazi
Crecent Sembuli,kiongozi wa Mradi wa ubunufu wa dira hizo za maji kutoka chuo hicho, amesema lengo kubwa la ubunifu huo ni kuboresha ukusanyaji mapato na kuzuia upotevu wa maji
Amesema bado wanaendelea na shughuli za ubunifu ili kuboresha zaidi,kama unavyofahamu shughuli za ubunifu ni shughuli ambazo ni endelevu , kwa hiyo tunaendelea kushirikiana na Ruwasa ili kuboresha miundombinu
Anna Maimu mkazi wa Sanya juu, amesema jambo hilo ni nzuri,kwani itakuwa muarubaini ya wasoma mita wasio waaminifu wanakuwa na tabia ya kuwabambikia bili wananchi.
Amesema pia hata kwa wale watu wenye tabia ya kumia maji kwa hivyo watajifunza ,tunnampongeza aliyebuni utaratibu huo.
Mwishos