Na Geofrey Stephen Arusha .
TRA NA HALMASHAURI ZA ARUSHA ZATAKIWA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WAFANYABIASHARA.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameitaka Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Arusha pamoja na Halmashauri zinazounda mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wafanyabiashara wa Mkoa huo na kujiepusha na bugudha na ukusanyaji wa kodi za dhulma.
Mhe. Makonda amebainisha hayo Usiku wa Ijumaa, Februari 21, 2025 kwenye Tuzo za Mlipakodi bora wa mwaka 2023/24 mkoa wa Arusha, Hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mount Meru Jijini Arusha, akiipongeza TRA pia kwa kuendelea kupunguza malalamiko ya kikodi kutoka kwa wafanyabiashara.
Katika sehemu ya Hotuba yake Mhe. Makonda kando ya kuisifu Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa mwaka 2023/24, amewataka wadau wa makusanyo ya serikali kuendelea kujenga mahusiano mazuri na walipakodi ili kuhakikisha kuwa wanawakuwa sababu ya Biashara kukua badala ya kufa kutokana na sababu mbalimbali.
Moja ya waliopata tuzo za mlipaji bora ni pamoja na Kampuni ya Hanspoul ya HANSPAUL AUTOMECHS LIMITED ya Jijini Arusha (Automotive Ltd ) ambao wamekua washindi wa pili ikiwa ni kwa mara nyingine wakipata tuzo ya mlipaji bora wa kodi .
Ataivyo Kamaljit Singh Hanspaul
Hanspaul Group Chairman wa kampuni hiyo ya hasnpoul akizungumza na vyombo vya habari ametoa rai kwa wananchi na wafanya biashara wengine kua na tabia ya kulipa kodi mara kwa mara kwani taifa linajengwa kwa kodi za maendeleo na sio vinginevyo
Mwisho.