Na Mwandishi wa A24tv.
Viongozi wa Dini Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro,wameombwa katika nyumba zao za ibada wasisahau kuhubiri kuhusu ukatili dhidi ya watoto kwani limekuwa tatizo kubwa wazazi wakishughulisha zaidi kutafuta fedha na kusahau watoto wao
Hayo yamesemwa na Mkuu wa kituo cha Polisi Sanya Furaha Mwakajila ,kwa niaba ya Mkuu wa Polisi Wilayani Siha Zakia Shuma, wakati Akizungumza katika Maazimisho ya maridhiano day yaliyofanyika katika ukumbi wa hospital ya wilaya hiyo.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo,ameomba Viongozi wa Dini kuwahubiria Wazazi wanapokuwa katika kujitafutia kipato wasisaha namna ya kuwalinda watoto dhidi ya ukatili
“Ni kweli swala la watoto Sasa hivi ni janga kubwa kumekuwa na unyanyasaji mkubwa kwa watoto uku Wazazi wakiwekeza katika kutafuta fedha”amesema
Amesema kitu kinachochangia sana katika mkoa huu Wazazi wapo bize sanakutafuta Hela, wakati mwingine hauelewi hizo pesa wanamtafutia nani
Amesema Wanamuacha kule yupo katika. Mazingira ambayo hayana usalama,yeye yupo ametingwa anatafuta pesa , sasa hizi pesa sijui anamtafutia nani
Nadhani sisi kama Viongozi tuwakumbushe Wazazi kama wanavyotafuta pesa ,lakini wakakikishe familia yao ipo salama ,watoto wamewaweka katika hali ya usalama
Sisi tuneshuhudia uko West Kilimanjaro mji mwema watoto wameungua ndani ya nyumba,watoto wadogo wameachwa nyumbani wenyewe,mkubwa ana miaka 4, mwingine 3 na mwingine 2
Watoto wameungua ndani ya nyumba Wazazi hawapo ,wameenda kutafuta ridhiki ,wamewasha kiberiti moto ukawaka ndani huyo wa miaka 4 alifanikiwa kutoka
Kwa hiyo tuendelee kuwakumbusha Wazazi kuhusu ulinzi wa mtoto ,fanya kila kitu ,lakini Kwa faida ya mtoto.
Aidha Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka , amesema mbali ni ukatili dhidi ya Watoto kuna changamoto ni nyingi migogoro ya kudhulumiana mali hasa kwenye maswala ya mirathi na Aridhi
Akitolea mfano kwamba kuna shauri la mama kufuzwa kwenye nyumba aliyekuwa akiishi na mume wake kwa miaka zaidi ya kumi watoto wamekwenda kumtoa,wewe na nani,mtoto hawezi kumpangia baba yake aishi namna gani
Kinachotakiwa ni kushauri ,sasa hii bado ipo kwenye jamii yetu,naomba jamuiya hii ya maridhiano kutilia mkazo tusione ni jambo dogo ni jambo ambalo linaweza kuvuruga amani tukemee, tuendelee na jitihada hizi
Mwisho