Hai,Wakazi wa Masinonda,Mungushi kati,Kona ya Karungu na Majengo Kijiji cha Mungushi Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro,wanalazimika kucha usingizi na kuamka saa nane za usiku kupata maji safi na salama
Huduma hiyo ya maji wanayapata kutoka katika Bodi ya Maji ya losaa Kia
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, wamesema jambo hilo limekuwa kero kubwa na inasababisha maendeleao kurudi nyuma.
“Ni kweli inarudisha juhudi za maendeleao nyuma kwani muda mwingi wanawekeza kutafuta maji safi na salama badala ya shughuli za maendeleao”wamesema Wananchi hao,
Jackison Mbasha mmoja ya Wananchi hao mkazi wa eneo la Majengo, amesema maji yanapatika kwa wiki mara moja ,tena siku ya jumatatu
Amesema kutokana na madhila hayo ,hivyo kulazimika kwenda kutafuta maji maeneo mengine au hata kununua ya kisima ambayo sio salama kwa matumizi ya kunyws kabla kwa kufikia na kuwa mifugo
“Ni kweli yanapatikana kwa wiki mara moja tena siku ya jumatatu ,siku nyingine hakuna inakubidi kwende maeneo mengine au ukanunue ya kisima na kusababisha kuacha shughuli za kujiingizia kipato amesema Mbasha
Marta Porospa mkazi wa mtaa wa Masinonda , pi amesema maji yamekuwa changamoto hasa kipindi hiki yanatoka usiku wa saa 8 ,wakati mwingine unapata kidogo haya todhelezi inabidi ukanunue maji ya kisima
Changamoto nyingine ukitumia maji bili inakuja shilingi 5000 au 6000,lakini wakati mwingine maji hakuna na umechota mara mbili Kwa mwezi bili inakuja shilingi 100,000.
Hivyo lile swala na kumtua mama ndoo kichwani bado changamoto katika eneo hili,Labda kwa ushauri labda Sasa wachimbe visima kama vyanzo vya maji vinakuwa na upungufu wa maji
Meneja wa Bodi ya losaa Kia, Jerry Jose, amekiri kuwepo kwa changamoto hizo ,ambapo amesema wanakabiliana navyo ili kuhakikisha watu wanapata maji bila usubufuamesema,
Amesema kwa mfano maeneo ya kona ya karungu na Mumbai wanapata maji kwa mgao kutokana na hali ya kiangazi maji yamepungua kwenye vyanzo vya maji,kuna Mradi upo itasaidia kuondoa tatizo hilo utaanza na maeneo mengine pia upo mradi
Kwa upande wa meneja wa Ruwasa Wilayani humo, Emanuel Mwampashi, Akizungumza swala hili la ukosefu wa maji maeneo ya Kingereka a ,Dorcas,mlima shabaha , amesema kwamba kuna mgao
Amesema hali hiyo inatokana na kiangazi kilichopo , mvua hazikunyesha masika madogo vyanzo vya maji uko mlimani vyanzo maji yamepungua hivyo kusababisha hali ya mgao
Mwisho