Na Geofrey Stephen .Arusha
Kongamano kubwa katika Kuelekea siku ya wanawake duniani, limedanyika Jijini Arusha huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stagomena Tax amewataka wanawake kuzitendea haki nafasi mbalimbali wanazozipata, akizitaka asasi za kiraia kutoa fursa sawa katika utendaji.
Dkt. Stagomena ametoa kauli hiyo Machi 06, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano Nyasa Hall cha jijini Arusha , ikiwa no shamrashamra za kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, ambayo kitaifa yatafanyika Machi 08, 2025 Jijini Arusha, mgenirasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya michezo vya sheikh Amri Abeid.
Waziri Tax pia ametoa wito kwa sekta binafsi kutoa fursa za hadhi na mazingira salama kazini kwa wanawake kwenye sekta ya utalii nchini, akihimiza pia jamii kupambana na ukatili wa kijinsia ambao mara nyingi umekuwa ukirudisha na kuwaacha nyuma wanawake kwenye maendeleo.
Waziri Stagomena amehimiza wanawake kujiongeza na kutumia fursa mbalimbali zinazotengenezwa na serikali, akihimiza ushirikiano kati ya wanaume na wanawake katika nyanja zote, kwa kiwango sawa na malengo bora katika kufikia maendeleo ya wote.
Mwisho.