Siha,
Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Christopher Timbuka,katika kuelekea uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu,amewataka watu wanaokusudia kufanya mchakato wa kuchaguliwa kuwa Viongozi wakati ukifika ,kudumisha umoja,upendo na amani kwa wanasiha na watanzania wote
Haya amesema March 28 2025, wakati wa futari iliyoandaliwa na ofisi ya Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi Kwa ushirikiano na ofisi ya mkuu wa Wilaya katika Msikiti wa SanyaJuu kiwilaya humo.
Akizungumza mara baada ya waumini kupata futuri hiyo, amewataka watu hao wanakusudia kwenye mchakato wa kuchaguliwa kudumisha amani na upendo , ambapo iliudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali,Viongozi wa dini,na madiwani
“Ni kweli tunawakaribisha wote wanaotaka kuja wakati ukifika,kikubwa ninachotaka kwao ni kudumisha umoja upendo na amani kwa wanasiha na watanzania wote”amesema Timbuka
Timbuka amesema hayo ndiyo maombi yake kwa watu ambao wanakusudia kufanya mchakato wa kuchaguliwa kuwa Viongozi katika Wilaya hiyo
Amesema bila ya kuwa na amani hakutakuwa na maisha mazuri,hata shughuli zetu za kiuchumi zitadorora,hata sisi Viongozi,tunafarijika tukipata mahali tunaona Wananchi wanafurahi kwa pamoja,wanafanya shughuli pamoja.
Sisi Wilayani yetu ni wamoja ,kwa hiyo tunatakiwa kuwa wamoja na kuendelee kudumisha amani hasa kipindi hiki ambacho tunaelekea uchanguzi, tuendelee kushikamana
Timbuka ameendelea kusisitiza kwamba kwa sababu Viongozi hao wanatafuta nafasi ya kuongoza,wanataka kuwaongoza binadamu hawa hawa,wanasiha hawa hawa, sasa kama hakuna amani hawa wanasiha utawaongozaje,sio tunachotaka na amani
kwa upande wake Wilfrend Kileo Mangi kutoka Wilayani Siha ,amewaonba Waislamu kuendelea na maombi wakati wa mwisho wa mfungo huo wa Ramadani,wazidi kuweka kwenye maombi uchanguzi wa mwaka huu 2025,uwe wa amani.
Tuiombee na Dunia pia kwa sababu vita vikizuka ulaya wakitumia makombora hata Ile hewa chafu itafika mpaka uku kwetu,Kwa hiyo tudumu katika maombi
Awali sheikh wa Wilaya hiyo Abubakar Hashimu ameshukuru Rais Samia Suluhuu Hassani,kwa kutuletea Viongozi wa Serikali katika Wilaya hiyo wanaolinda maslahi ya watu wa Siha ni ,wametukutanisha hapa kweny futuri ni jambo zuri
“Ni kweli ni jukumu letu kuwashukuru Viongozi wetu akiwamo Mkuu wa Wilaya Christopher Timbuka na Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri Haji Mnasi bila kusahau kijana Tumsifu Kweka ambaye na yeye alikuwa wa kwanza kufuturusha,wamepata ujira wa kufuturisha,
Mwisho