Na Mwandishi wa A24tv .
Polisi kata NGARENARO jijini Arusha Mkaguzi Msaidizi wa polisi TADEY TARIMO ametoa rai hiyo kwa wanafunzi wa shule za msingi na secondary katika kata hiyo wakati akitoa Elimu juu miradi mbalimbali ya polisi jamii.
A/INSP TARIMO amewataka wanafunzi kutokua na hofu waonapo viashiria vya vitendo vya ukatili dhidi yao au kwa watu wao wa karibu na badala yake watoe TAARIFA mapema ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Sambamba na hilo Mkaguzi huyo amewahakikishia Usalama wanafunzi hao pindi watoapo TAARIFA za Ukatili na uhalifu mwingine unaotokea na kutendeka katika maeneo yao.
Mwisho A/INSP TARIMO amewataka wanafunzi kuepukana na tabia ya utoro na badala yake wasome kwa bidii na kuzingatia masomo ili waweze kufikia malengo yao!