Siha,
Wananchi wa kijijii cha Sanya Hoyee Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wameomba Viongozi wa maeneo hayo kuzuia upigwaji Muziki katika baar ambazo hazina sehemu maalumu ya kuzuia sauti(Sound proof)ili kuepusha usumbufu kwa jamii
Maombi hayo yamekuja baada ya kuwepo upigwaji wa mziki mkubwa na kusababisha kero hasa nyakati za usiku ambapo watoto, wagonjwa, pamoja na wanafunzi kushinda kupata usingizi
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, wameomba wausika kufunga vyombo hivyo maalumu vya kuzuia sauti.
“Ni kweli kero kubwa wanashindwa kupata usingizi , Watoto, wagonjwa wazee na wengine,Muziki unapigwa Baar na hata baadhi ya nyumba za ibada ,ni usumbufu mkubwa”wamesema Wananchi hao
Julius Msaya mkazi wa kijijii hicho eneo la Mabanzini, amesema wamekuwa hawatamani usiku ufike kutokana kero hizo za mziki na hata baadhi ya nyumba za ibada nazo zimekuwa chanzo cha kelele kwa matumizi ya vyombo vinavyotoa sauti kubwa
“Ni kweli Baadhi ya nyumba za ibada ambazo kimsingi zinahitajika kwa ajili ya huduma za kiroho,zimeamua kukiuka Sheria na kuwa chanzo cha kelele kufuatia matumizi makubwa ya vyombo vinavyotoa sauti kubwa ,hivyo kuwa kero kwa majirani , tunaomba Serikali iingilie kati jambo hili”amesema Julius
Julius amesema kikubwa tunachoomba waweke vizuia sauti ili waendelee na majukumu yao ili kuepusha usumbufu huo
Mwenyekiti wa kijijii hicho Mosses Munuo,amekiri kuwepo kwa kadhia hiyo,na kusema kwamba hata yeye mwenyewe halali hapati usingizi kutoka na kelele hizo
Munuo amesema walishapiga marufuku lakini bado tabia hiyo inaendelea ,hivyo kuomba wanatoa leseni ni vizuri wakafika kwenye vijiji ili kufahamu mazingira jinsi yalivyo
Kwa upande wake mtendaji wa kijijii hicho Hashimu Issa, amesema kwamba wenye hizo Baar alisha wahi kuwafungiwa na baadaye akawafungulia ,
Nashukuru kwa taarifa tutalishughulikia ikiwa ni pamoja na Baadhi ya nyumba za ibada zenye kuleta kelele
Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC),kanuni ya uthibiti wa sauti na mitetemo ya mwaka 2015
imetolewa maelekezo ya viwango vya sauti vinavyoruhusiwa kwenye makazi inatakiwa isizidi decibels 35 ,lakini kwenye makazi na biashara ni decibels 45 kuanzia kuanzia saa 6 mchana
Pamoja na kanuni hiyo, lakini imebainika kuwa kelele hupigwa hadi kufikia kati ya decibels 78 hadi 100 na kuleta adha na usumbufu kwa majirani
Mwisho