Na Bahati Hai,
Waumini wa Dini ya kiisllamu mkoani Kilimanjaro,wametakiwa kuendelea kudumisha amani katika kuelekea uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu
Hayo yamesemwa March 31 2025,na sheikh wa mkoani Shaabani Mlewa wakati wa Maadhimisho ya sikukuu ya Eid Elfitir iliyofanyika Msikiti wa Safii Bomang’mbe Wilayani Hai mkoani hapa.
Akizungumza na waumini hao mara baada ya swala hiyo ya Eid ,amewataka Waislamu kuendelea kudumisha amani na upendo kwani ndiyo msingi mzuri wa maisha
“Ni kweli uchanguzi mkuu unakuja,na kila uchanguzi unapokuja uinakuja na vitimbwi vingi , sasa akili kichwani,wewe mwenyewe kama muislamu inatakiwa kuwa wa kwanza kutunza amani”amesema Mlewa
Amesema uisilamu ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu, muislamu ndiyo anakuwa wa kwanza kuchunga amani,asitokee mtu akakushawishi kutaka Nchi haikaliki wewe mwenyewe utakosa pakukaa.
Piga hesabu unamali zako fujo ikiingia hakuna kinachosalia ,akili za kupewa changanya na za kwako,kwa hiyo nawaomba sana mlinde amani,
angaliebi Nchi za jirani wanavoteseka ,watu wanachinjana wanauana
Aidha katika uchanguzi ujao amewataka Wananchi kuchagua Viongozi wazuri , ambao watawaongoza mnaowaamini,na nyinyi wenyewe ingieni kwenye uchanguzi mchaguliwe
Tupate watu tutakao waamini,watakao tusaidia ,tunaitaji maendeleao,ukienda Kwa Mwenyekiti wa kijijii kusiwe na ukirutumba ,nataka kumuonea Mbunge anakata simu hapana,tunataka Viongozi wazuri wasema ukweli.
Awali Immamu wa Msikiti huo, Athumani Hamis,amesema lengo la funga hii ni kwe mwenye kufunga kufikia daraja ya kuwa mcha Mungu ,afanye yale aliyoamrishwa na Mola wake na kuacha yale aliyokatazwa na Mola wake
Hivyo kuwasii waumini kuendelee kufanya mema kama tuvyokuwa tunafanya ndani ya mfungo huu wa Ramadhan,kwani kurudi kufanya maovu ni jambo baya sana mbela ya Mwenyezi Mungu naunahesabika umepata hasara.
Mwisho