Na Bahati Siha,
Serikali Wilayani Siha mkoani imetakiwa kuwa makini na watu wanajitokeza kupanda miti sehemu mbali mbali, Wilayani humo kwani baadhi yao wanaopanda miti hiyo uitelekeza bila kuipatia matunza ili ikuwe
Hivyo kutakiwa kuonyesha mpango kazi wao wakuitunza miti hiyo mpaka ikuwe ndiyo waruhusiwe kupanda miti hiyo.
Haya yamesemwa na Wananchi wa kata ya Ngarenairobi wakati wa zoezi la upandaji miti eneo lao shule ya Sekondari Namwai na chanzo cha mapato cha madini ya moromo West Kilimanjaro,
Wananchi hao ,wakizungumza mara baada ya zoezi,wametaka kuonyesha mpango kazi wao wakuitunza miti hiyo tabia hiyo kupigwa na Wadau wote wamazingira ili tija ya upandaji miti iwezo kuonekana
“Ni kweli lazima waonyeshe mpango kazi wao hi itabia ya kupanda miti nakutokomea ni sawa na kujionesha kwamba na weo wamepanda miti,hapana,” wamesema Wananchi hao
Ni lazima tuungane kama kweli tuna nia ya dhati ya kutunza mazingira kumuunga mkono Rais Samia Suluhuu Hassani nikuitunza miti yote iliyopandwa hadi ikuwe wametilia mkazo Wananchi hao
Yakubu Saidi mkazi wa eneo hilo, amesema kwa muda mrefu ipo tabia wa Watu na hata taasisi za Serikali na Watu binafsi,wamekuwa na khulka ya kupanda miti na kutokomea na kuacha miti hiyo bila uangalizi ,jambo ambalo sio zuri
Amesema hii tabia haitafikia lengo la kutunza mazingira, ndiyo sababu tukasema wanajitokeza kataka kupanda miti watuonyeshe na mpango wao wakuitunza hadi ikuwe ,hapo kweli watakuwa na nia ya dhati ya kutunza mazingira
Afisa mazingira wa Wilaya hiyo Hermenegild , amesema lengo ni kupanda miti zaidi ya 1 milioni mwaka huu maeneo mbalibali katika Wilaya hiyo yakiwamo ya uwazi
Kwa siku ya leo Ofisi ya Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri kwa kushirikiana na wakala wa madini na TFS wameweza kupanda miti kwenye chanzo cha mapato cha madini ya moromo na shule ya Sekondari Namwai, ambapo wameweza kupandia miti 2000.
Ambapo pia amewaonye wafugaji sehemu iliyopandwa miti kuacha kupeleka mifugo ,kwani Sheria itachukuliwa dhidi yao
Mwisho