Siha,
Jumuiya ya Wanawake wa chama cha mapindizi (UWT), Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro,imesema itawaunga mkono Wanawake wote watakaojitokeza kugombea nafasi yeyote ya uongozi ikiwamo ya udiwani na ubunge katika uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyiwa mwaka huu
Haya yamesemwa na Mwanaidi Kalegela katibu wa( UWT) , Wilayani humo katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani march 6 2025,ambopo kiwilaya yalifanyika katika ukumbi wa RC SanyaJuu ,na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka.
Akizungumza katika Maazimisho hayo, amesema (UWT) wapotayari kuwaunga mkono Wanawake watakajitokeza kugombea nafasi ikiwamo ya udiwani na ubunge
“Ni kweli sisi kama jumuiya ya Wanawake kazi yetu ni kuhakikisha tunawaunga mkono watakaojitokeza kugombea nafasi mbali mbali ya uongozi katika uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyiwa mwaka huu wakatusemee changamoto zetu tulizonazo”amesema
Amesema amelazimika kusema hayo, kwamba halmshauri ya Siha ina kata 17 kati ya hizo Diwani 1 ndiyo aliyechaguliwa inaongozwa na mwanamke , hivyo amewataka kujitokeza kwa wingi muda utakapofika kugombea nafasi ili na wawe wengi na kusema mambo yao ya maendeleao.
“Ni kweli ukiangalia kata zote 17 ,16 zinaongozwa na madiwani wanaume,sasa hata changamoto zetu nani atatuwakilishia ndiyo sababu ya kusema tutawaunga mkono Wanawake watakajitokeza kugombea nafasi mbalibali”amesema Kalegela
Mwenyekiti wa Jumuhiya hiyo Bertha Mlay ,mbali na kuunga mkono Wanawake kugombea,amempongeza Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kuleta miradi mingi katika halmshauri,ikiwa ujenzi wa barabara,vituo vya Afya,miradi ya maji , vyumba vya madarasa na umeme
Kwa upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi, amesema halmshauri hiyo imekuwa ikitoa mkopo isiyo na riba kwa vikundi vya Wanawake na vijana wajasiriamali pamoja na walemavu
Ambapo halmshauri hiyo mwezi March mwaka huu inatarajia kutoa mkopo zaidi ya sh,500 milioni Kwa vikundi mbali mbali, hivyo wake mkoa wa kula.
Aidha Afisa maendeleao ya jamii Mark Masue, amesema Mbali na mikopo ya asilimia 10 ya Wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu ,pia halmshauri kupitia ofisi ya maendeleao ya jamii kuna mikopo ya wajasiriamali
Masue amesema sifa ya kupata mikopo hiyo lazima kwanza uwe na kitambulisho cha ujasiriamali, kuna fomu maalumu unajaza na unaandikiwa barua na Mtendaji wa kata au Kijijii ya kukutambulisha unalipia shilingi alfu ishirini unapata kitambulisho ambacho utakaa nacho kwa miaka mitano
Hii yote Rais Samia Suluhuu Hassani anataka kila mtu apate fedha ili aweze kufanya shughuli za kumuingizia kipato na kuendesha maisha ya familia yake na Taifa kwa ujumla
Mwisho