Siha,
Baraza kuu la Waislamu Tanzania ( BAKWATA), Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro limesema litampokea mtu yeyote yule anayekuja na jema ambalo lipo ndani ya Aya na hadidhi na kushirikiana naye bega kwa bega katika kuwaletea maendeleao ya Waislamu na jamii kwa ujumla.
Haya yamesemwa March 25 2025,na Sheikh wa Wilaya hiyo, Abubakar Hashimu wakati wa zoezi la ufuturishaji kiwilaya lililofanyika katika Msikiti wa SanyaJuu kiwilaya ambalo lilibebwa na Tumsifu Kweka mjumbe wa halmshauri kuu ya CCM mkoa na mkutano mkuu wa CCM Taifa
Sheikh Akizungumza mara baada ya zoezi hilo kuitimishwa , amesema Ofisi ya Baraza hilo Wilayani humo itampokea mtu yeyote yule anayekuja na jema kwa maendeleao ya Waislamu na jamii kwa ujumla
Abubakar amesema,alilolifanya Kweka ya kukusanya Waislamu wa Siha na watu mathehebu mengine na kuja kufuturu kwa pamoja ni muendelezo wake wa kila mwaka anatoa kiasi kiasi kugawa kwenye mashule ,kuna watoto wetu kule kwenye mashule wanaishi hostel , kuna shule kama sikosei zipo 8 pamoja na Ile ya mawasiliano ndiyo anavyofanya.
Safari hii ameona futar yake iende kwa utaratibu huu kwa kukusanya Waislamu wa Siha kwa wakati mmoja icho ndicho alichokipendelea ,nawaombeni Waislamu hapo tupo kwenye maswala ya ibada
“Sisi tutampokea maadamu hilo jema halipingani na Aya na hadidhi,tutalipokea nafikiri ndiyo wito wangu mkubwa,nanukuu tena ofisi ya Bakwata Wilaya ya Siha chini sheikh wa Wilaya nampokea mtu yeyote yule anayekuja na jema ambalo lipo ndani ya Aya na hadidhi “amesema Abubakar
Nafikiri mmenielewa ya kaisari mpa kaisari ,haya ni ya Mungu , Saumu ni ya Mungu,huyo ameamua kupata fungu kwa Mungu,Kuna mayatima wamekuja hapa wakala
Mwenyekiti wa Jumuhiya ya maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Wilayani humo Gerald Mollel, amesema Tanzania ni Nchi pekee Duniani ambaye imefanikiwa kusimamia swala la amani,kidini na kijamii,ni ngumu Nchi nyingine kukuta Waislamu na wakristo wanakaa pamoja na wanaweza kufuturu pamoja ni jambo la kipekee
Ndugu zangu dumisheni amani hii iendelee , lakini niwapongeze Waislamu katika ibada hii ambaye mnaendelea nayo ya mfungo,ni kama hatari kwa mwanadamu kuacha kula , ndiyo maana ukifika hospital unaambiwa jitahidi sana kula ,lakini nyinyi mmeweza kuacha kwa siku 30 Mungu awaepo neema na heri
Mollel amesema,hata katika bibilia Yesu aliambiwa na wanafunzi wake mbona tumejaribu kukemea pepo na hazijatoka,Yesu akawaambia namna hii haiwezekani Ila kwa kufunga na kuomba,niwatakie wakati mwema wakati mnaenda kukaribia kumaliza mwezi huu na Mungu awabariki
Kwe upande wake Tumsifu Kweka amesema ,kipindi hiki tunaelekea kwenye uchanguzi mwaka huu, niwaombe sana Viongozi wa Dini kutumia frusa hiyo kuliombea Taifa,tumtangulize Mungu,tumuombee Rais Samia Suluhuu Hassani atuongoze kutuvusha katika kipindi hiki
Wanasiha wenzangu kwa pamoja, kubwa sana tusaidiane,tushikamane,tuwe wamoja ni muhimu sana,tukipata frusa kama hii tuliyopata leo tumefuturu pamoja bila kujali Dini zetu ,umoja wetu ni nguvu yetu
Aidha Wilfrend Kileo Mangi kutoka Wilayani humo, amesema nje ya mfungo kama ibada ya kufikia daraja ya kuwa mcha Mungu ,pia funga inakufanya kuwa na afya njema Kwa mujibu wa watu wa Afya , niwapongeze Waislamu kwa ibada hii
Mwisho