Hai ,
Kanisa la Adventista Sabato Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ,litaendelea kutoa mafunzo kwa vijana wa marika tofauti katika kanisa hilo, kwa lengo la kuwalea vijana katika maadili yenye nidhamu na kuwajengea uwezo wa kumbapana na maswala ya ukatili dhidi ya watoto
Haya yasemwa March 16 ,2025 na Ezekiel Elisante kiongozi wa vijana Kanda ya Kilimanjaro wakati wakati wa Maadhimisho ya matendo ya huruma kila mwaka mwezi March,ambapo huwatoa huduma ya kurudisha fadhila zao kwa jamii kupitia matendo ya huruma , kwa kufanya shughuli za kijamii, ambao walifanya usafi kituo cha Polisi Bomang’ombe
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilisha shughuli hizo za usafi , amesema Kanisa limekuwa na idara mafunzo ya vijana kwa muda mrefu kwa ajili ya kujitolea kutumika katika jamii.
“Ni kweli kanisa letu limekuwa na idara ya vijana kwa muda mrefu likitoa mafunzo mazuri ikiwa ni kundi ambalo limeandaliwa kama vijana kwa ajili ya kujitolea kutumikia jamii kwa kuwa na maadili mema hasa kutokana na kila siku kusikia matukio ya udhalilishaji watoto”amesema Ezekiel
Amesema mafunzo hayo yamekuwa msaada kwa vijana, hasa kwa Duniani ilipofikia kwa sasa kila muda unasikia habari za ukatili dhidi ya watoto huyo amebakwa huyu amekawitiwa nilazima kuwajengea vijana uwezo ili wawe na uwezo wa kupambana na mambo hayo
Ezekiel ametaja makundi hayo ya ,Vijana yanayopata mafunzo kuwa yamegawanyika katika makundi kadhaa,kundi la kwanza kuanzia miaka 4 hadi 9,hawa wanamafundisho yao,miaka 10 hadi 15,wanamadusho yao kulingana na umri wao
Pia amesema wapo wa miaka 16 hadi 22 pia wanamandifusho yao ,haya ni makundi ambayo wanakuwa katika umri wa ujana na pia wanamadundisho yao,
Miaka 23 hadi 35 ni vijana ambao wanawafundisha kuwalea Watoto wadogo kama tulivyowagawa katika makundi niliyokuwa nimeyataja mwanzoni
Hawa vijana wamefundishwa namna ya kuishi na raia namna ya kuwa Wakristo waaminifu katika jamii na vijana wengi wamebarikiwa kutokana na mafundisho haya na Kanisa limefanya hivi kwa muda mrefu
Ukiona kwamba wanatunza mazingira,wanakuwa raia wema waaminifu ni sehemu ya mafundisho hayo wanafundishwa Kanisa ,hivyo kuomba taasisi nyingine kutomafunzo kama hayo kuendelea kuwajengea uwezo vijana ili Taifa libaki salama
Kwa upande wake Elias Mkwizu Mwenyekiti wa kaya wa Kanisa hilo,ameitaka jamii kufanya matendo mazuri,ili watoto waweze kuiga matendo hayo,kuna matendo ya ufutaji bangi,unywaji wa pombe sio mambo mazuri watoto kuiga yanaharibu nguvu kazi ya Taifa ,hivyo tunaomba jamii inadilike
Mkuu wa kituo cha Polisi Bomang’ombe Magdalena Raymond ,amewashukuru waumini hao kuona umuhimu wa kwenda kufanya usafi katika kituo hicho, ni jambo jema kuwafundisha vijana kujali mazingira
Awali Yusufu fransis,ambaye kiongozi idara ya vijana wa Kanasi hilo ,mesema katika Juma hilo ambalo lilianzia tarehe 8 mwezi wa tatu hadi tarehe 15 mwezi wa tatu 2025,
Ambapo wamekuwa walifanya shughuli za kijamii sehemu mbali mbali ikiwamo kununua kalamu,dafutari nguo za shule kwa watoto wahitaji pia kuchungia damu kwa wahitaji ,ambapo walitoa uniti 24
Mwisho