Na Bahati Hai,
Wanakikundi cha jamiiyatul Akhaaqul Islamia (JAI) kutoka Msikiti wa Nuur Bomang’ombe Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wameujumuika kwa pamoja na wagonjwa wa Hospital ya wilaya hiyo kusherekea sikukuu ya Eid Elfitir kwa kupata chakula cha mchana kwa pamoja
Haya yamesemwa na Mwenyekiti wa kikundi hicho Hussein Maulid Akizungumza na waandishi wa habari hospitalni hapo, kikundi hicho kipo katika Msikiti wa Nuuru Bomang’ombe kilianzishwa mwaka 2021 ,kwa lengo la kusaidia watu wenye uhitaji ,
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo kukamilika , amesema ni ibada kubwa kuwatetwagonjwa na kujumuika pamoja kupata chakula ni sadaka iliyo njema na nzuri.
“Leo tumekusanyika hapa kwa ajili ya kushirikiana na ndugu zetu wagonjwa waliopo hapa Hospitalini pamoja na wauguzi ,tumeona watakuwa wapweke siku kama hii ya Eid ambaye ni siku ya furaha tupate chakula kwa pamoja”amesema Hussein
Tumeona tusfurahi mwenyewe na wenzetu wapo katika hali ya matatizo ya kuumwa ,kwa hiyo tumekuja kushirikiana nao ili na wao wafarijike,kwa hili kama alikuwa anaumwa aone tumekuja kuwatembelea,hiyo peke yake inaweza kumpa nafuu
Hussein ,amesema hilo zoezi sio kama nila sikukuu ya Eid pekee,ni zoezi endelevu,kila wiki siku ya jumapili uwe wanafika hospital hapo kwa ajili ya kutembea wagonjwa kufanya Dua,kuwapa chai na mahitaji mbali mbali
Kama nilivyosema awali lengo la kundi hili ni kujitolea na kusaidia wahitaji na pia ni tabia ya kiisllamu ya kudaidia watu wenye uhitaji
Aidha kama kuna mtu amekwama matibabu kwa ajili aidha ya vipimo,dawa hata damu labda hana mtu wa kumtolea damu , basi tunachukua jukumu lake kuweza kumsaiidia kufikia maisha yake
Festo Munisi, mmoja ya wagonjwa walipata chakula hicho,na kupata frusa ya kuongea amewapongeza kwa kuona umuhimu wa kutembea wagonjwa ni jambo la nzuri na kuwaomba waendelee na moto huo ,kwani wagonjwa wanahitaji furaja.
Diwani wa kata ya Bomang’ombe Wilayani humo Evod Njau , amesema jambo jema kujitolea na kujumuika kupata chakula na wagonjwa ni jambo jema na la kuungwa mkono na watu wa mathehebu mengine wanatamiwa kuiga tabia hii
Sio lazima kusubiri msaada kutoka ulaya au uarabuni,tunaweza sisi kusaidiana jamii yetu,kwa hiyo niwapongeze sana na tunaendelea kuwaunga mkono
Mwisho