Siha,
Jumuhiya ya watumia maji mto Sanya Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, wamesema elimu ya mazingira wataendelea kuitoa hata sehemu ambazo tayari wameshatoa ili kuondoka sintofahamu ya watu kudai elimu hiyo haijawafikia na kuendelea kuharibu mazingira
Mwenyekiti wa Jumuhiya ya watumia maji mto Sanya ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya mto Pangani Moshi ,alipotembele vyanzo vya maji Kijijii cha Ashengai Kata ya Karansi na kukuta baadhi ya vyanzo hivyo kugeuzwa sehemu ya kilimo hivyo kuwa hatarini kukauka.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada kutembea vyanzo hivyo likiwamo Timbiga la kweka na ,chemchem ya makiwia, amesema watajikita zaidi kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wasipate kutoa visingizio kwamba hawajapata elimu hiyo
“Ni kweli tutajikita zaidi kuendelea kutoa elimu,kuna watu wanalima na kuharibu vyanzo hivyo ukiwauliza wanakwambia wao hawajui kama kufanya hivyo ni kosa licha ya kuwepo na vibao vya maonyo vilivyowekwa na elimu kutolewa”amesema Moshi
Moshi amesema kutokana na changamoto iliyopo hapa ,watapendekeza kuweka alama bikoni ili waweze kufahamu mipaka yao na mwisho wao ni hapa ili kulinda maeneo hayo
Amesema,lakini kabla ya kuweka alama hizi, wataendelea kutoa elimu ya mazingira kata nzima ya Karansi ,inatosha kwa jamii kufahamu kwamba mita 60 hazitakiwi kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo hivyo
Elimu hiyo itasaidia kuepuka wasipate kisingizio kwamba hawana elimu ya mazingira ,kuna kibao tulikiweka hapa chemchem ya makiwia lakini walikuondoa kwa sababu kilikuwa kinasema ni mafuruku kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji ndani ya mita 60,hii sio sawa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijijii hicho Isaya Mollel amesema baada ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa kijijii hicho,walikaa kwa pamoja na kukubaliana kujua mipaka ya Kijijii hicho.
Baada ya kufahamu mipaka na maeneo ya wazi changamoto waliyokutana nayo ni watu wamevamia maeneo ya vya maji ikiwamo matindiga kufanya shughuli za kilimo hivyo kutishia vyanzo hivyo kukauka
Tunataka kuyaresha matindiga na chemchem hizo na kupanda miti ili kurudisha uoto wa asili ili kumuunga mkono Rais Samia Suluhuu Hassani kulinda mazingira na kuwapa vikundi vya vijana ,kina mama na wezee wawezo kufuga samaki kama kitega uchumi katika maeneo hayo
Meisho