Siha,
Mkuuu wa Wilaya siha mkoani Kilimanjaro, Christopher Timbuka amevitaka vikundi vilivyopata mikopo ya Halmshauri,kutumia mikopo hiyo kwa malengo walioainisha ili kufikia malengo waliyokusudia
Kauli hiyo ameitoa Mei 23,2025 wakati akikabidhi mfano wa hundi ya zaidi ya sh,300 milion kwa vikundi 46 katika ukumbi wa halmshauri hiyo
Akizungumza mara baada ya kukabidhi mfano huo wa hundi ,amevitaka vikundi vilivyopata fedha hizo,kwenda kutumia fedha hizo kwa malengo makhususi
” Kama mnavyofahamu Wilayani hii ipo kwenye Wilaya za 10 za majaribio katika utoaji mikopo,,niwajibu wetu kufanya vizuri ili na wengine wa Wilaya zingine waweze kuiga “amesema Timbuka
Amesema nimatumaini watakwenda kutekeleza kama walivyoomba ,na mikopo hii haina riba,wairijesha kwa wakati ili na wengine waweze kupata mikopo hiyo,tunawashukuru Bank ya uchumi katika kushirikiana kutoa mikopo hii
Kwa hiyo Rai yangu kubwa kwa watu waliokopa kutumia mikopo hii kwa malengo waliyoainisha kwenye maombi yao,ili waweze kupata fedha za kurejesha
Kwa upande wake Dancani Urasa Mwenyekiti wa halmshauri hiyo,amempongeza Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnas kwa ukusanyaji mapato ya ndani mzuri
Amesema kwa sababu hiyo asilimia 10,inayotolewa inapatikana kutokana na makusanyo hayo ya ndani ,ndiyo maana tumewaza kukuposha fedha hizo mikopo
Aidha Mkurungenzi huyo , amesema anamshukuru Rais Samia Suluhuu Hassani, kwa kuruhusu utoaji wa mikopo hii kwa Wananchi wetu
Leo tumefanikiwa kutoa kiasi cha sh,300 milioni kwa vikundi hivyo vilivyotajwa baada ya wiki mbili zinatarajiwa kutolewa kwa vikundi vingine kiasi cha Zaidi ya sh,300 milioni zingine.
Samwel Adu Afisa Mtendaji mkuu wa bank ya uchumi, amesema kwa kushirikiana na halmshauri,wametoa elimu ya fedha kwa wanufaika wa vikundi 48 katika awamu hiyo ya kwanza
Anasema unafahamu ukimpa mtu hela bila kumjuelisha anaweza asiitumie kwenye kusudio alilopanga kufanya,tunatoa elimu ya fedha kwa wale wanakikundi kuwa na nidhamu ya fedha
Pamoja na elimu kutolewanaendelea wataendelea kuwa karibu kufuatilia kuhakikisha kwamba fedha zinatumika katika lengo lililokusudiwa
Kaale lukundo mmoja ya wanufaika wa mikopo hiyo, amesema wanaishukuru halmshauri kwa mikopo hiyo na kuahidi kutekeleza yale yote ya kurejesha kwa wakati
Mwisho