Na Mwandishi wa A24tv.
WADAU wa utalii zaidi ya 800 kutoka nchi zaidi ya 40 Duniani wanatarajia kushiriki maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibu-Kilifair, yanayotarajia kufanyika katika viwanja vya Magereza kuanzia juni 6-8 Mwaka huu Jijini Arusha.
Maonesho hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka jijini hapa,yamelenga kutangaza na kukuza utalii hapa nchini na yanatarajia kukutanisha makampuni mbalimbali zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya nchi:
Shoo aliongeza kuwa maonesho hayo yatakuwa na manufaa makubwa kwa washiriki kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali hapa nchini ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuleta watalii nchini kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Alisema kampuni yake imefanikiwa kupitia matamasha mbalimbali kuwakutanisha wadau wa utalii wa hapa nchini na nchi za ulaya lengo likiwa ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini Kimataifa.
Kwa upande wake ,Mkurugenzi Mtendaji KKF,Tom Kunkler amesema kuwa,maonesho ya mwaka huu yamelenga utalii endelevu ndani ya Karibu -Kilifair ambapo kwa kulenga mustakabali wa mazingira, wameanzisha mpango wa “Uendelevu wa Utalii” kwa kutumia vifaa vya mbao, vibuyu vya maji, utenganishaji wa taka na maeneo ya kuchakata chupa. Haya ni baadhi tu ya hatua kuelekea maonesho ya kijani ya siku zijazo.
Baadhi ya wadhamini wa maonesho hayo,meneja wa hoteli ya nyota tano ya KIBO PALACE GROUP , Hashim Mohamed alisema kuwa wao kama miongoni mwa wadhamini wamejipanga kupitia hoteli ya KIBO PALACE kuwapokea na kuwakarimu wageni mbalimbali watakaofika katika hoteli hiyo kwa ajili ya huduma za malazi.
Naye mmoja ya wakurugenzi wa Kibo Palace, Beatrice Laswai,alisema wamejiandaa kikamilifu kuhakikisha wageni wanapata huduma nzuri na bora ya malazi kutokana na umaridadi wa vyumba vya kulaza wageni.
GG “Katika viwanja vya maonesho tutakuwa na banda letu la maonesho ambalo litatambulisha huduma zote zinazopatikana katika hoteli ya KIBO PALACE na wale watakaokosa huduma zetu hapa Arusha tuna hoteli nyingine ilipo Moshi Mkoani Kilimanjaro” 55.
Tumejiandaa kikamilifu kutoa huduma bora mwaka huu. Katika uwanja wa maonyesho, tutapatikana kwenye kibanda T5. Kwa wale wanaotafuta malazi, tunatoa chaguzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na hoteli yetu kuu ya Arusha, pamoja na vyumba na nyumba za kifahari mjini Moshi,” alisema Laswai.
Mwisho.