Na Geofrey Stephen . Arusha
Wananchi wa jiji la Arusha wametakiwa kufanya usafi katika Mazingira yao yanao wazunguka bila kushurutishwa na kama wakishindwa maafisa mazingira wachukue hatua kwao kwa mujibu wa sheria kuwatoza faini ya shilingi Elfu hamsini .
Akiongoza zoezi ilo leo mapema katika maeneo ya Soko Kuu Jijini Arusha na Stendi kubwa katibu Tawala wilaya Arusha Jacob Julius Rombo amesema ni jambo la kushangaza sana siku ya kufanya usafi katika jiji la Arusha alafu wanatokea wananchi wachache kutokushiriki ni jambo ambalo sio la kizalendo kwani jambo hilo nilakitaifa kwa kila mwananchi .l
Jumamosi,ya leo tarehe 31/05/2025 imekuwa ni siku ya uzinduzi wa Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani,ambapo Kimkoa,Arusha imeadhimisha kwa kufanya Usafi wa Mazingira katika maeneo Makuu Mawili,Soko Kuu na Stendi Kuu.
Katika zoezi hilo ambalo lilianza majira ya saa kumi na mbili asubuhi,Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha,Ndg. Jacob Julius Rombo kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania,amewapongeza Wananchi wote.
waliojitokeza kufanya usafi wa mazingira katika maeneo tajwa na kusisitiza kuwa lazima Wananchi wawe na desturi ya kufanya usafi wa mazingira….”Mazingira lazima yawe safi kwa afya zetu,na ili yawe safi lazima sisi Wananchi tuyasafishe…alisema Ndg. Rombo”
Aidha,Ndg. Rombo ameshangazwa na baadhi ya Wananchi wasiopenda kushiriki kufanya usafi wa mazingira na kusema sheria ndogo ndogo za Jiji lazima zitumike ili kurahisisha uratibu wa zoezi la usafi Mkoani Arusha.
Kwa upande wao Wananchi waliojitokeza wamepongeza utaratibu huo wa kuhimiza kufanya usafi wa mazingira hasa maeneo hayo ya kufanyia biashara kwani ni sehemu muhimu ya kujipatia kipata ambapo bila usafi biashara hudorora.
Maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yatafanyika tarehe 05/06/2025, ambapo kitaifa yatafanyika Jijini Dodoma na Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Tanzania.
Mwisho .