Na Bahati Siha,
Baraza la Madiwani halmshauri ya Siha mkoani Kilimanjaro,limekusudia kutangaza utalii wa ndani uliopo katika Wilaya hiyo ili kuwavutia watalii wengine kufika kujionea maliasili zilizopo na kuchangia pato la Taifa
Kauli hiyo imetolewa na Dancani Urasa Mwenyekiti wa halmshauri hiyo,baada ya Afisa utalii wa (TFS)kupewa nafasi ya kuzungumza kuhusiana swala la West kili forest tour challenge 2025 ,, linatarajiwe kufanyika June 21 hadi 22 2025 inakwenda sambamba na kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Wilayani humo
Akizungumza kwenye Baraza hilo ambalo liilikuwa la kuwasilisha taarifa za kata, amesema ni muhimu Madiwani na Wadau wengine kutangaza utalii uliopo katika Wilaya hiyo
“Ili ni jambo jema sana ,kwa maana ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Siha ,sisi kwenye sekta ya utalii bado tupo nyumba sana ,tuhamasishane “amesisitiza Ndancan
Dancani amesema Wilaya ya Siha imebahatika kupata vivutio vya utalii vingi,lakini kuna vituo vingine ambayo watu hawafahamu , hivyo hatuna budi kuvitangaza ili watalii waweze kupata taarifa na kufika kwa wingi
Vincent Kileo Diwani wa kata ya Endument,mmoja ya madiwani hao ambaye ameunga mkono kutangaza vivutio hivyo, ambapo amesema pia ni juhudi za kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhuu Hassani swala la utalii
Awali Afisa utalii wa (TFS)Mensieur Elly ,katika taarifa yake, amesema June 21 hadi 22 2025,kutakuwa tukio la kuhamasisha utalii,ambalo linaenda kwa jina West kili forest tour challenge 2025 ,itakayafanyoka ndani ya hifadhi ya msitu wa West Kilimanjaro
Ambapo amesema kutakuwa na matukio kutembea kwa miguu kwenye maeneo mbalibali ikiwamo kwenye vivutio vya utalii,maporomoko ya maji,maeneo ya kuogelea,mapango ya asili,kuona wanyama wa ndani ya hifadhi ya msitu, kuona ukanda wa Shira
Mbali na hayo pia kutakuwa na Mbio za baiskeli ndani ya msitu wa asili pikipiki na michezo ya riadha,i sambamba ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhuu Hassani ili kuongea idadi ya utalii ndani na nje ya Nchi
Mwisho