Hai ,Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Bomboko,amewataka Wananchi wenye nyumba za kupanga Wilayani humo wanapofanya maamuzi ya kupangisha,wawapangishie watu wanaowatambua ili panapotokea tatizo liwezo kutatuliwa bila kikwazo
Haya yamejiri kwenye ziara ya Mkuu huyo wa kwa lengo la kuzungumza na Wananchi pamoja na kusiliza kero kata ya Bomang’ombe mtaa wa Gezaulo
Akizungumza kwenye mkutano huo ambapo pia umehudhuriwa na Diwani wa kata hiyo pamoja watumishi wa halmshauri,amewataka wamiliki wa nyumba hizo kuzingatia swala hilo la utoaji taarifa ili kuepuka kukamatwa.
“Ni kweli tunaweza kukukamata kwa sababu hautoi taarifa,upo utaratibu wa wageni wanapofika sehemu kutambulishwa kwa Viongozi wa Serikali ili kufahamu walipotoka,ili kesho na kesho kutwa panapotokea tatizo likiwamo la wezi pasiwepo na usumbufu wa kuzitatua”amesema Bomboko
Bomboko amesema kwamba mmoja ya kero ni iliyosemwa hapa ni wenye nyumba za kupanga,kuwapokea watu na kuwapo nyumba bila kutoa taarifa kwa Viongozi wa Serikali za mitaa
Amesema ni wajibu wenye nyumba hizo,kuhakikishe wanaowatambua kwa kupata barua kutoka mabalozi, balozi anakufahamushe huyu ni mtu namtambua ,saa nyingine mtu anafika hamtambui mnampa hifadhi akifanya tukio na kukimbia inakuwa vigumu kumpata
Kwa hiyo Watendaji wa kata zote 17 za Wilaya hii na Viongozi wengine waanze utaratibu wa kuwatambua wageni wanakuja kwenye maeneo yao kwa mujibu wa utaratibu
Awali mmoja ya Wananchi hao Neema Tarimo, amesema kero yake ni watu wenye nyumba kupokea wapangaji pasipo kutoa taarifa au kuwatambulisha kwa Viongozi wa Serikali za mitaa hii ni changamoto.
Akitokea mfano hivi karibuni kuna kijana anakaa maeneo ya hapa Gezaulole,amepangasha kwenye nyumba moja ,amekuwa akifanya matukio ya wezi kiiba vitu kutoka maeneo mbali mbali nakuifanya Ile nyumba kuwa Danguro la kuhifhia vitu hivyo
Aidha Wananchi wa eneo hilo wamempa pongenzi Mkuu huyo wa Wilaya kwa kufika katika eneo lao kwa lengo la kuwasikiliza na kero na kuzitatua kwa kuipatia ufumbuzi
Mwisho