Masomo ya sayansi, teknolojia,uhandisi na hisabati (STEM) yanawezesha wanafunzi kupata ujuzi na maarifa yanayosaidia kujitegemea ikiwemo kutatua changamoto za jamii zinazozunguuka
Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Tumaini Senior ,Modest Bayo katika mahafali ya kidato cha sita ambapo jumla ya wanafunzi 56 walimaliza shule katika fani mbalimbali ya sayansi na masomo mengine.
Mkuu wa shule hiyo, Sifael Msengi amesema shule hiyo inatoa mafunzo ya sayansi jamii , biashara na masomo mengine kwani wamekuwa wakifanya vema huku akisisitiza ushirikiano mzuri kati ya wazazi, walezi, walimu pamoja na wanafunzi kwa kuweka mikakati ya kufanya mitihani kwa wingi ya ndani na nje ikiwemo kumaliza topiki za masomo kwa wakati