Hai,
Mkuu wa Wilaya Hai mkoani Kilimanjaro Hassani Bomboko amewataka Viongozi wa kata ya Bomang’ombe Wilayani humo kufanya kila liwezalo kuwabaini wahalifu na kuwahukulia hatua za kisheria
Hayo yamejiri kwenye mkutano uliofanyika mtaa wa Gezaulole Bomang’ombe , ulioandaliwa na mkuu huyo wa Wilaya ,kuongea na Wananchi maswala ya maendeleao pamoja na kero , moja ya kero zilizoibuka ni wezi na ulevi uliokithiri eneo hilo.
Mkuu huyo wa Wilaya akizungumza mara baada ya kuongea na Wananchi hao,ametaja Viongozi wa kata hiyo akiwamo Polisi kata kuhakikisha ulinzi na usala kwa raia na mali zao
“Mmesikia mambo ya watu wanavunjiwa ,wanakabwa na kuporwa , hapo Gezaulole hangaikeni na wahalifu,mmenisikia ,mfukishieni OCD,haya maelekezo yangu , hakikisheni mnakomesha uhakifu”amesema Bomboko
Bomboko amesema Wananchi hawawezi wanakaa, wanaishi kwa mashaka mashaka wakati waliopewa dhima ya kuhakikisha usalama wapo ,fanyeni kila muliwezalo kuwabaini wahalifu wote na wachukuliwe hatua.
Kama mmeshazungumza nao na bado watu wanakwepuliwa wanakabwa,mazunguzo hayo hayana tija tena,chukueni hatua za kisheria watafuteni wakamatwe
Polisi kata umenielewa na mkafanye vikao vya kata vya ulinzi. na usalama, Mtendaji wa kata ndiyo yalikuwa maelekezo yangu , lakini mpaka leo na hali ya usalama ndiyo hivyo mkakae vikao,Tarafa unanisikia,sitarajii kurudi hapa kwa ajili ya haya mambo
Sambamba na hilo ametoe rai kupunguza unywaji ulipindukia ili kutunza afya, Viongozi wa Kiroho mtusaidie kwenye nyumba za ibada kukemea mambo haya yanayohusu ulevi ili kulinda nguvu kazi ya
Taifa
“Ni kweli nawaombeni sana viongozi wa Kiroho uku kwenye nyumba za ibada mtusaidie kukemea ,unyweji pombe uliopitiliza umekuthiri , nguvu kazi ya Taifa inapungua kutoka na unywaji huo,amesisitiza Bomboko
Aidha kero nyingine ilikuwa mbwa kuzagaa hivyo mitaani nakuanza kuuma watu,ambapo ametaka maafisa mifugo kuhakikisha mbwa wote wanaozurura mitaani kupigwa risasi, baada ya watu kadhaa kuumwa na mbwa mtaa Gezaulo
Awali Okili Kimaro mmoja ya Wananchi walifika katika mkutano huo katika kero aliyoitoa hapo , amesema wanaishi kwa wasi wasi kutokana na wimbi la vibaka wanaowaibia watu nyakati za usiku na mchana,
Amesema,wapo vibaka wanatembea na pikipiki usiku na kuwapora mikoba na simu Wanawake,wapo wanavunja nyumba za watu mchana wakiwa makazini na wapo wanavunja nyumba nyakati za usiku kwa kweli hali sio salama kabisa,wanarudisha maendeleao nyuma
Pamoja na Wananchi wa eneo ili kutoa taarifa kwa Viongozi wa maeneo haya pamoja na Polisi kata ,bado wezi umekuwa ikiendelea ,tunashuru Mkuu wa Wilaya kufika hapa tumemuekeza kero zetu ambapo amesema anasema anazifanyia kazi.
Diwani wa kata hiyo Evord Njau , amesema kikao kilifachofanyika cha Mkuu wa Wilaya ni mizuri,amesikiliza kero,yapo mambo mengine aneyatolea maagizo,tunaamini yatatekelezwa kwa wakati
Niombe Wananchi kwa namna ya kipekee kabisa,wanapoitwa kwenye mkutano kama hii ,wajitokeze , kwa sababu Viongozi hao ni wateule wa Rais ili waje kutusaidia.
Mwisho