Zikiwa zimesalia siku mbili Mbunge wa Jimbo Siha mkoani Kilimanjaro Godwin Mollel,amewataka Wananchi kujitokeza kutumia frusa kufika Hospital ya wilaya hiyo kwa ajili ya kupata vipimo vya macho na magonjwa ya Wanawake bila gharama yeyote.
Zoezi hilo limeandaliwa na Taasisi Mo Dewji foundation kwa kushirikiana na Dr Godwin Mollel foundation.
Akizungumza mara baada ya kufiki hospital hapo, amewataka Wananchi kujitokeza kwa mwingi na kutumia frusa hiyo kabla muda haujafikia mwisho
“Ni kweli muda ni mchache watu wanitokeze kufanya vipimo na kupata matibabu ,watumie hii frusa , mpaka sasa watu zaidi ya 3000 wameshapata huduma”amesema Mollel
Amesema zoezi hilo limeanza Mei 3 na linatarajiwe kufikia mwisho Mei 5 ndiyo maana nasisitiza kujitokeza kupima na kupata matibabu bila gharama
Mollel amesema Mo Dewji kwa ajili ya maswala ya matibabu mbalibali Nchini nzima anekubali kutoa sh,35 billion,katika maeneo mengine, lakini kwa Wilaya ya Siha nimemuomba sh,800 milioni
Amesema kwamba matibabu ni bure,wale watakaofanyiwa opeeresheni watatibiwa bure ,wale wenye watoto ambao wanamgongo wazi wamezaliwa na wenye kichwa kikubwa wanahitaji kupelekwa Hospital ya Muhimbili watatibiwe bure
Kwa hiyo nawaomba nendeni uku nyumbani waambieni watu wengine wajitokeze wake kupata vipimo na kupata matibabu,hata wenzetu wa Wilaya za jirani ikiwamo Hai,Arumeru na Longindo wafike kupata huduma.
Mollel amesema kwamba muitikio ni mkubwa, wagonjwa ni wengine,tutaongeza madakitar kutoka Hospital ya Mwenzi ili kuweza kuwahudumia kwa haraka
Pia amesema wakati zoezi la upimaji likiendelea ametikea mtoto mwenye ugonjwa sikoseli ugonjwa huu unatibika Rais Samia Suluhuu Hassani ametushogezea huduma karibu,mtoto atasafurishwa ili kupata matibabu atahudumiwa na atapona , mpaka sasa kwa Wilaya ya Siha wameshatibiwa Watoto watatu
Mganga Mkuu wa hospital hiyo,Paschal Mbotta, amempongeza taasisi hiyo kwa ushirikiano na Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuona umuhimu wa kuleta msaada huo katika hospital hiyo,wahitaji ni wengi na wengine waige mfano huu
Awali Amina Ramadhani ambaye ni mratibu wa Mradi huo, amesema mwaka jana walifanya zoezi ili kwa kuweka kambi kama Wilaya tisa,
Amesema Mbunge wa Jimbo ili Godwin Mollel ii pamoja na majukumu mengine baada ya kuliona hilo aliomba lifanyike katika Jimbo lake, ambapo alimfuata Muhammad Dewji pamoja na Mkurungenzi ili zoezi liweze kufika Wilayani Siha na kufanikiwa
Mwisho