Na Geofrey Stephen Arusha
Mkuu wa Wilaya Mstaafu ,Joshua Nassari ni miongoni mwa wanachama 28 waliochukua fomu kuwania ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki.
Nassari alisema kuwa ana udhoefu wa ubunge na anauwezo wa kujenga hoja hivyo wana Arumeru Mashariki ana hakika changamoto zao huenda zimepata mgombea sahihi kwani yeye sio mgeni Bungeni bali anarudi kwa awamu ya pili kuendeleza alipoishia ili aweze kuunganisha wananchi wa Meru kwa wamoja kwa nyakati zote.
Alisema yeye ameombwa kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Arumeru Mashariki na sio vinginevyo hivyo ana imani na chama chake na yuko tayari kutumwa kufanya kazi katika jimbo hilo kwa maslahi ya wananchi wa Jimbo hilo.
Mwisho
Like this:
Like Loading...