Na Bahati Hai
Mganga mkuu wa Hospital Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Itikija Msuya metoa shukurani kwa Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kuwapatia fedha sh,900 milioni kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya Hospital
Hayo yamo kwenye taarifa ya Mganga huyo wakati akisoma taarifa yake wakati wa mbio za Mwenge ulipo tembelea Hospital
Akisoma taarifa hiyo June 4,2025, amesema Hospital katika mwaka wa fedha 2022/2023,ilipokea kutoka Serikali kuu fedha kiasi cha sh,900.miloni kwa ajili ya Utelezaji wa miradi mbalibali ili kuboresha huduma za Afya
Ametaja miradi hiyo ni pamoja ujenzi wa jengo la la maabara, ujenzi wa jengo la famasia, ujenzi wa jengo la wodi daraja la kwanza na ujenzi wa njia ya kupitisha wagonjwa zenye urefu wa kilometa 1 na upanuzi wa wodi ya wazazi
Msuya amesema Mradi hiyo itakuwa na faida mbalimbali ,ikiwa ni pamoja ufanisi wa mawasiliano kutoka jengo moja kwenda jingine ,umeboreshwa, mazingira ya utoaji wa huduma yamekuwa rafiki kwa watumishi hasa kwa uwepo kwa njia za kupitishia wagonjwa.
Msuya amesema mapato ya hospital yameongezeka hasa baada ya wodi daraja la kwanza (Grage one Ward),kuanza kutoa huduma
Kutokana na hayo hatuna budi kumshukuri kwa Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kuwapatia fedha hizo ambazo zimewezesha uboreshaji wa miundombinu na kupandisha hadhi ya Hospital kama ilivyosemwa awali
“Ni kweli ni muhimu kutoa shukurani ,kwani fedha ni nyingi sana zimeletwa Kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbali mbali ikiwamo ya Afya kama tunavyoona’amesema Msuya
Awali Mkuu wa Wilaya hiyo Hassani Bomboko, katika taarifa yske aliyeitoa wakati wa kupokea Mwenge Uhuru ,amesema kwamba Mwenge huo utakagua miradi 7, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi yenye thamani zaidi ya sh,3 billion
Mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD)kituo cha Afya kata ya Kia,kuweka jiwe la msingi, ujenzi wa Barabara ya shabaha,0.59 km Kwa kiwango cha lani Kata ya Muungano,kuweka jiwe la msingi
Ujenzi wa famasi ,maabara, upanuzi wa wodi daraja la kwanza na uzii wa njia za kupitishia wagonjwa, Bomang’ombe, uzinduzi
Ujenzi wa shule ya msingi sadala ,masama kusini , uzinduzi,Mradi wa maji kikavu soka kwa sadala , kuweka jiwe la msingi na Mradi wa ujenzi wa jengo la biashara Kirewe na matumisi ya nishati safi, Bomang’ombe uzinduzi
Kwa upande wake baada ya kutembelea miradi hiyo Kiongozi wa wakimbiza Mwenge kitaifa Ismaili Ussi, ametoa kongole kwa ujenzi mzuri wa miradi hiyo.
Nimpongeze Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri Dios Myinga kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa miradi mbali mbalimbali katika halmshauri hii
Tumeona miradi yote tuliyotembela ipo vizur kwa asilimia 100 ndiyo maana tumeithibisha ,kwa kweli nyinyi ni miongoni mwa Wilaya mliotajwa kufanya vizuri,jipigieni makofi
Ambapo pia alisisitiza kauli mbio kujiandaa kushiriki uchanguzi mkuu wa mwaka 2025,kwa amani na utulivu
Mwisho