Na Mwandishi wetu Siha,
Mkazi wa Kijiji cha Wandri Wilayani siha mkoani Kilimanjaro,Agust Shoo (baba Steven)(59)amehukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha maisha jela,kwa makosa mawili la kubaka na kulawiti mtoto wa miaka (6)
Hukumu hiyo imetolewa julay 15 ,2025 ,na Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Jasmine Abduli,ambao kesi hiyo likuwa na mashahidi watano akiwamo muhanga mwenyewe, Daktar na mama wa mtoto huyo, kesi hiyo namba 20095/2023
Mbapo kosa la kwanza kubaka ni kifungu 130 (1)(2)(e)na kifungo 131 (1)cha Sheria ya makosa ya jinai sura 20 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022 ,adhabu jela miaka 30
Kulawiti kinyume na kifungo 154 (1)(a)cha Sheria ya makosa ya jinai,sura ya 16 ilivyofanyiwa marejekebisho 20222 ,adhabu yake jela maisha
Mwendesha mashitaka wa sherikali David Chishimba,mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo,amesema mshitakiwa alifanya tukio hilo kwa nyakati tofauti , October 8 ,2019 .katika Kijiji hicho huku akitambua kufanya hivyo ni kosa
Alikuwa akimuingilia Binti huyo mbele na nyuma,Binti na anasoma darasa la kwanza shule mmoja Wilayani humo,
hivyo anaporejea nyumbani huwa kutoka shuleni anakuwa mwenyewe nyumba
wakati huo bibi akienda kwenye mihakangaiko ya kutafuta riziki , mshitakiwa alikuwa akitumia frusa hiyo kumuadaa na kwa zawadi na kumfanyia ukatili kwani walikuwa ni majirani
“Ni kweli mtoto huyo ,alikuwa akiishi na bibi yake na alikuwa akisoma darasa la kwanza,anaporudi nyumbani anakuwa yupo pekeyake,bibi yake anakuwa kwenye mihangaiko,hivyo mshitakiwa kwa sababu walikuwa majirani anatumia nafasi ya kufanya unyama huo”amesema David
Mwendesha mashitaka alisema jambo hilo liligundulika shuleni ,ambapo mtoto huyo alifika shuleni katika hali isiyo ya kawaida ,haja kubwa ikitoka wenyewe,watoto wenzie wakimcheka
Taarifa hii ikamfikia mwalimu ndiyo alimchukua na kufanya naye mahojiano ,ambapo alifunguka na kumtaja mshitakiwa ambaye alikuwa jirani yao
Baada ya ushahidi huo Mahakama hiyo iliridhika ma ushahidi huo usiacha shaka ndani yake na ili iwefundisho kwa wengine ,unakwenda kutumikia kifungo cha maisha jela
Mwisho