Na Richard Mrusha
MAMLAKA ya Serikali Mtandao (eGA) ni taasisi ya serikali iliyopewa jukumu la kuratibu na kusimamia matumizi ya TEHAMA ndani ya taasisi za umma. Kupitia teknolojia, eGA inalenga kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Katika utekelezaji wake, eGA imebuni na kusimamia mifumo mbalimbali ya TEHAMA inayorahisisha upatikanaji wa huduma za serikali kwa njia ya kidijitali ukiwemo mfumo wa e-Mrejesho
unaomwezesha mwananchi kutuma maoni, mapendekezo au malalamiko kuhusu huduma anazopata kutoka taasisi za serikali. Maoni hayo yanaweza kutumwa kwa njia tatu.
Hayo yamesemwa jana na Meneja Mawasiliano wa eGA Subira Kaswaga wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda la eGA kwenye maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba wakati akizungumzana waa dishi wa habari ambapo kpitia simu kwa kupiga *150*00#, kisha kuchagua namba 8 na kufuata maelekezo au kpitia tovuti: www.e-mrejesho.gov.go.tz na kkpitia app ya e-Mrejesho inayopakuliwa kwenye simu ya mkononi mwananchi anaweza kutuma maoni.malalamiko au hata pongezi kwa serikali.
Kaswaga amesema ubora wa mfumo huo umejidhihirisha baada ya kushinda tuzo ya kimataifa katika kipengele cha Serikali Mtandao (e-Government) kwenye Mkutano wa Dunia wa Jumuiya ya TEHAMA – World Summit on the Information Society (WSIS 2025).
“Tuzo hii ni ushahidi kuwa Tanzania imetambuliwa duniani kwa ubunifu wa kiteknolojia unaowezesha mawasiliano kati ya serikali na wananchi kwa uwazi na uwajibikaji mkubwa,
“Mfumo huu umewekwa miongoni mwa mifumo bora duniani kwa kuwa unahamasisha ushiriki wa wananchi katika utawala na kuchochea uwajibikaji ndani ya taasisi za umma.
Vile vile amesema eGA imejenga mifumo mingi huku alitaka baadhi kuwa ni pamoja na Mfumo wa M-Gov: Hutoa huduma mbalimbali za serikali kwa njia rahisi kupitia simu za kawaida bila hitaji la intaneti. Kupitia *152*00#, wananchi hulipia huduma kama umeme, maji na nyinginezo.
Amesema mfumo mwingine ni Mfumo wa Kubadilishana Taarifa Serikalini: Huwezesha taasisi za serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa kidijitali kwa haraka na usalama, hivyo kuokoa muda na gharama kwa wananchi.
Pia amesema upo Mfumo wa Usalama kwa Akaunti za Serikali: Uthibitisho wa mara mbili (Two-Factor Authentication) unaimarisha usalama wa taarifa na akaunti za serikali kwa kutumia simu za mkononi kama nyenzo ya ziada ya uthibitisho.
Kupitia mifumo hii, eGA inaendelea kuweka msingi imara wa serikali ya kidijitali, inayowajibika na inayoweka wananchi mbele. Wananchi na taasisi zote za serikali wanahimizwa kutumia kikamilifu mifumo hii ili kuboresha huduma, kuongeza uwazi na kujenga serikali ya kisasa inayojali wananchi wake.