Na Mwandishibwa A24tv Siha .
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Reneal international Education Outreach imetoa vifaa vya Teknojia ya habari na mawasiliano (Tehama)Kompuyta katika shule nne za Sekondari Wilayani siha mkoani Kilimanjaro.
Makabidhiano hayo,yamefanyika katika shule ya Sekondari Matadi iliyopo Wilayani humo, nakuhudhiriwa na viongozi mbali mbali ikiwamo wakuu wa shule na maafisa Elimu kata.
David Nyangaka afisa taasisi hiyo, akizungumza wakati wa Kukabidhi Kompuyta hizo kwa Katibu tawala wa Wilaya hiyo Jane Chalamila ,ambaye alikuwa mgeni rasmi ,kwa niaba ya mkuu wa Wilaya Christopher Timbuka,anetaka vifaa lhivyo kutunzwa na kuleta matokeo mazuri
“Ni kweli vifaa hivi ni muhimu nilazima vitunzwa Ili viweze kudumu Ili kuleta matokeo mazuri”amesema Nyangaka.
Nyangaka amesema lengo la taasisi hiyo,imetambua umuhimu wa Tehama na ndiyo sababu ya kuamua kuunga mkono juhudi za Serikali kuhusu somo hilo.
Amesema anaamini vifaa hivyo watavitumia na kusaidia maendeleo ya shule,nakufanya vizuri zaidi ,na kwamba mpaka sasa wameshazifikia halmshauri 35 Nchini
Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Said Athumani , katika kauli yake ameahidi kutunza vifaa hivyo vifaa hivyo na kuongeza ufanisi katika somo la Kompuyta.
Amesema wadau wametoa vifaa hivyo Ili kuimarisha kujifunza na ufundishaji kwa kutumia teklojia hiyo ya tehama
Naye Katibu Tawala huyo Jane Chalamila ,aneishukuru taasisi hiyo,kwa msaada walioutoa na kwamba usomaji wa kipindi kile haukuwa kana hii,ulikuwa mgumu,frusa hii mliopata muitumie vizuri huo,nakuomba wanafunzi
Awali Afisa elimu Sekondari Wilayani humo Naomi Swai katika taarifa yake, amesema,Somo tehama limekuwa Moja wapo ya vipaumbele vya kisekta yenye lengo la kuharakisha maendeleo ya Nchi
Kuanzia mwaka 2012 , Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknojia ilianzisha mpango kufundisha matumizi ya Tehama kwa shule za Msingi na Sekondari.
Amesema mwaka 2022, Serikali kupitia Wizara ya Tamesemi iliwapatia walimu wote vishikwambi na mwaka 2023/2024,halmshauri ilipatiwa computer 100 ,ambazo zilisambazwa katika shule za Sekondari
Mwaka 2024/2025,kupitia maombi ya Afisa elimu Sekondari kwa mdau wa elimu David Nyangaka,wamepatiwa Maabara nne za Tehama,
Ambazo zitakuwa katika shule za Sekondari Namwai,Oshara,Sanya juu na Nuru, laptops mpya 20 kwa kila Shule,Maabara hizi 4,ni awamu ya kwanza,lengo ni kupatiwa Maabara za aina hii katika shule zote katika halmshauri hiyo
Naomi amesema pamoja na frusa zilizotajwa hapo juu,bado kuna changamoto katika kutekeleza mtaala wa Tehama.
Upungufu wa Walimu na wataalamu wa Tehama, katika shule za Msingi na Sekondari, upungufu mkubwa vyumba vya tehama katika shule hizi
Kutokuwa na huduma ya uhakika ya internet katika shule hizo,kwani nyingi hazijaunganishwa katika Mkonga wa Taifa wa mawasiliano
Kutokuwa na Maabara za kisasa za Tehama na baadhi ya vifaa vilivyopo shuleni vimepindwa na wakati
Mwisho