Na Mwanfishi wa A24tv Hqndeni
Mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 297 umezinduliwa rasmi leo katika kijij cha Kwedizinga,
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, ukitarajïwa kuwahudumia zaidi ya wananchi 4,486, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mheshimiwa Salum Nyamwese, aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Balozi Dkt. Batilda Burian.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mh. Nyamwese alieleza kuwa mradi huo ni matokeo ya ushirikiano wa dhati kati ya Benki ya ABSA Tanzania na Shirika la World Vision Tanzania, akitoa shukrani kwa taasisi hizo kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuleta maendeled ya maji safi na salama kwa wananchi.
Mh. Nyamwese alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi thabiti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau wote wa maendeleo kwa lengo la kuimarisha huduma za kijamii na kupunguza changamoto za wananchi.
Aidha, aligusia kwa hisia taarifa kwamba wazo la kuanzishwa kwa mradi huo lilitokana na sauti ya mtoto wa kike, Binti Shania, jambo alilolieleza kuwa ni funzo muhimu kwa viongozi
kusikiliza sauti za wananchi na kuwatambua watoto kama sehemu ya maamuzi ya maendeleo.
Katika kuimarisha uendelevu wa miradi ya maj, Mh.
Nyamwese aliwataka viongozi wa Wilaya, Kata na Viji
kuhakikisha usimamizi madhubuti wa miradi hiyo, huku
akisisitiza kuwa RUWASA iendelee kutoa msaada wa
kitaalamu na kujenga uwezo wa Bodi za Watumiaji Maji
(CBWSOs).
Alimalizia kwa kutoa wito kwa wakazi wa Kwedizinga kuwa walinzi wa mradi huo kwa kuudumisha, kuutunza na kuuhifadhi kwa ajili ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
Mwisho .