Na MwandishinA24tv .
Katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 10 ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mgeni Rasmi Mheshimiwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akiambatana na Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Ridhiwani Kikwete, waliongoza zoezi la utoaji wa tuzo kwa waajiri na wadau waliotoa mchango mkubwa katika safari ya WCF.
Tukio hili ni ushuhuda wa mshikamano baina ya serikali, sekta binafsi na jamii katika kuhakikisha haki na ustawi wa mfanyakazi wa Kitanzania
Kampuni ya A-Z Goup LTD ya Jijini Arusha imeibuka kidedea mara baada ya kupata tuzo mbili nzito
Kuwa kampuni yakwanza kuwa na mfumo madhubuti wa usalama mahari pakazi na tuzo yapili yakuwa kampuni yakwanza kwakutowa taarifa za hajali kwa wakati
Pia kwa kupunguza ajali kazini mwajiri mkubwa ambaye anachangia na kujali usalama mahala pa kazi na kuwasilisha taarifa za wafanyakazi kwa wakati , pamoja na kua na mwajiri mwenye kuonyesha mikakati ya maboresho ya Afya mahala pa kazi .
A- Z imeshinda tuzo hizo kwa katika usiku wa kilele cha Miaka 10 ya Maadhimisho ya WCF iliofanyika Jijini Dar Es Saalam July 4 Mwaka 2025 .
Mwakilishi wa A- Z Group Meneja usalama Afya na Mazingira Eng. Harryson Rwehumbiza alikabidhiwa tuzo hizo mbili na Mgeni Rasmi Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ambapo pia amepongeza A- Z Group LTD kwa kutoa huduma nzuri na kuchangia taarifa za wafanyakazi kwa wakati na kuzitaka taasisi zingine kuiga namna makampuni makubwa yalivyo na mchango kwa watumishi wake.
Mwisho.