Na Doreen Aloyce, Dodoma
Mbunge viti maalimu Mkoa wa Pwani Subira Mgalu amesema kupitia Bajeti ya kilimo iliyopitishwa na Bunge ya zaidi ya Bilioni 970 mwaka 2023/2024 inaenda kuleta unafuu kilimo chenye tija kwa wakulima.
Kauli hiyo ameitoa Bungeni Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari juu ya bajeti ya kilimo ambayo imekuwa na ongezeko inapaswa kutekelezwa kwa maslahi mapana ya wananchi na jamii kwa ujumla.
Mbunge Subira amesema kuwa bajeti hiyo imepitishwa bila kikwazo kwani imeleta matumaini ambapo imewahusisha vijana kupitia program ya building better tommorow(BBT) na kati ya waliochaguliwa ni wasichana na kuwamilikisha ardhi .
” Sekta ya kilimo inatoa chakula inatoa ajira na zaidi ya asilimia 70 wamejiajiri kwenye kilimo , hivyo kupitia uongozi wa Samia Suluhu Hassani tumeona mapinduzi na ongezeko la bajeti kwa mara ya kwanza na tumeona manufaa kupitia mbolea ya Ruzuku zaidi ya bilion 292 imewasaidia wakulima. “Amesema Mbunge Subira.
Amesema kupitia uwezeshaji sekta ya kilimo hasa kilimo cha umwagiliaji itasaidia wananchi kupata chakula cha kutosha na kuondoa malalamiko mengi ya watanzania hususani bei ya vyakula.
“Dhamira ya serikali ya kuinua kilimo kuanzia mbegu,mbolea,umilikishaji wa ardhi ,umwagiliaji na ufufuaji wa mashamba inaenda kuleta tija kuelekea 2030 kuchangia asilimia 10 itatimia hivyo watanzania tuwe na matumaini. “amesema Mbunge Subira .
Katika hatua nyingine juu ya Mkoa wa pwani amesema kuwa wanayo furaha katika bonde la Mto rufiji wameanza kufanya upembuzi yakinifu kudhibitiwa mafuriko litakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi hekta laki nne kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kukamilika .
Mwisho.