Na Richard Mrusha Tabora
MKURUGENZI wa Biashara wa Asasi ya kusaidia sekta ya kilimo nchini (PASS TRUST) Adam Kamanda Amesema kuwa asasi hiyo inatoa dhamana kwa wakulima katika nyanja zote zinazoshughulika na kilimo cha mazao mbalimbali.
Amesema kuwa PASS TRUST imeanzishwa na Serikali ya Tanzania Kwa kushirikiana na nchi ya Denmark kwa lengo la kuondoa changamoto ya Wakulima hasa wadogo ambao hawana dhamana ya sheria ya fedha kama inavyohitaji ambapo sheria ya nchi inahitaji mtu yeyote anayechukua mkopo aweze kuwa na dhamana walau asilimia 25.
Mkurugenzi wa biashara wa asasi ya kusaidia sekta ya kilimo nchini Tanzania (PASS TRUST) Adam Kamanda akizungumza na waandishi wa habari
Kamanda aliyasema hayo Jana mkoani Tabora katika maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani ambapo kitaifa yanafanyaka mkoani humo , ambapo amesema kuwa kutokana na kuwepo Kwa changamoto dhidi ya Wakulima Serikali ya Tanzania na Denmark ikaanzisha PASS TRUST kama mfuko ambao uko chini ya Ofisi ya Waziri mkuu.
“Kwa kifupi lengo la mfuko huu na kazi yake ni kutathmini biashara, kutengeneza Mpango Biashara katika sekta ya kilimo kuanzia wavuvi, wafugaji, wa samaki,wakulima wadogo Kwa wakubwa kuwatengenezea mpango biashara kufanya tathimini na kuchukua mipango biashara hiyo kuiwekea dhamana.”alisema
Kamanda alifafanua kuwa dhamana hiyo inatolewa mpaka asilimia 60 Kwa jamii nzima lakini inatoa mpaka asilimia 80 Kwa miradi yote ambayo inahusisha wanawake, Vijana au inafanya kilimo kinachozingatia utunzaji wa mazingira na kuongeza kuwa katika hilo wanawake na vijana mara nyingi hawana dhamana hata wengine dhamana inakuwa ni kitu kigumu sana nakutolea mfano kuwa mtu anakuwa na nyumba haijapimwa labda haijafanyiwa tathimini na kwamba kupata asilimia 25 ni ngumu sana kwamba hiyo PASS TRUST ndiyo imekuwa na jukumu kubwa la kutengeneza miradi hiyo ya kilimo na kuipatia thamani.
Alisema kuwa mpaka hivi sasa Pass TRUST imeweza kufanya biashara Zaidi ya 66,000 na imeweza kutoa mikopo kwenye dhamana inayozidi takribani tirioni 1.5 mpaka Sasa hiyo ni karibu asilimia 25 ya mikopo yote ya kilimo inadhamana ya PASS TRUST.
Aidha mkurugenzi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania na Dennymark kubuni mfuko huo kwa sababu umechochea sehemu kubwa ya sekta hiyo ya kilimo, unafahamu Taasisi za fedha zinafedha lakini ni za wadau mbalimbali wanaowekeza na kwamba fedha hizo hazitakiwi kupotea kwa hiyo kama PASS TRUST inatembea na mkulima kila siku mkulima anapofeli na PASS TRUST imefeli.
“Kama mnavyo jua siku hizi kuna mabadiliko ya tabia nchi na miradi mingine inafeli kwa changamoto mbalimbali na hivyo tumekuwa tukilipa kwenye Taasisi za fedha miradi ambayo inafeli na tumekuwa tunatatua matatizo mbalimbali kwenye miradi iliyofeli vile vile na sisi kama PASS TRUST.
Nakuongeza kuwa ” Viwanda vinafeli wakulima malighafi zao zinapotea kwenye Viwanda lakini vile vile utunzaji wa mazao yote ni changamoto kwenye sekta ya kilimo ndiyo maana sisi PASS TRUST tumetia chachu tumeweka dhamana, tumefundisha wakulima, tumetengeneza vikundi vya wakulima tumeshiriki na ushirika na katika sekta yote tumeweka mkono wetu ili kuhakikisha wakulima wanafanikiwa,”
alisema Kamanda mkurugenzi wa PASS TRUST.
Aliongeza kuwa mpaka sasa Pass Trust inawanufika wanaozidi Milioni 3.4 nchi nzima katika dhamana hiyo na kuongeza kuwa pia wametengeneza ajira Million 2.7 hiyo ni hatua kubwa sana iliyofanyika kwenye sekta ya kilimo.
Alifafanua kuwa kwa kutambua changamoto kwenye sekta ya kilimo PASS TRUST pia imeweza kufanya mambo mengine mbadala katika sekta ya kilimo kwamba Moja kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, kusumbua sana nchini kuwa huwezi kujua mvua itanyesha lini ama jua litatoka kiasi gani tumeona wakulima mazao yao yakiwa yanaharibika hivyo ikaanzisha programu kijaniasha iliyosambaa maeneo mengi.
Alisema programu hiyo inamfundisha mkulima kilimo kinachozingatia usafi wa mazingira na uhai wa mazingira ukilinganisha na ongezeko la watu ni kubwa na kutolea mfano juzi tu watu walikuwa milioni 50 na Sasa ni milioni 60.
Pia Kamanda alisema kuwa changamoto wanazokutananazo kwenye kilimo biashara ni pamoja na wakulima kutokupata elimu ya kutosha kuhusu kilimo ukilinganisha kwamba kilimo kinahitaji uelewa wa kutosha na wakulima hawajui juu ya kuandika Somo mpango biashara hawajui mambo ya faida na hasara katika kilimo kutokana na hilo PASS TRUST inakuwa mbele kuwapeleka kwenye Taasisi za fedha.
Alisema changamoto nyingine nikwamba wakulima hawatunzi kumbukumbu pamoja na kuomba fedha nyingi ambazo hajui azifanyie nini badala yake anazipeleka kwenye miradi mingine isiyohusika.
“Mabadiliko ya tabia nchi ni tatizo sisi kilimo chetu bado kinategemea mvua na katika hayo kuongezeka Kwa jua ama mvua ama Majira kubadilika Kwa maana hiyo tunatoa dhamana kwa wale wa kilimo cha umwagiliaji
Kwa upande wa wanufaika wa Mradi huo Saraphina Jerad kutoka Mkoa wa Kigoma alisema kuwa huu ni mwaka wa Tano akinufaika na PASS TRUST na Jovitus Lumumba kutoka Tabora Igunga alisema kuwa PASS TRUST ni Shirika lililomsaidi kupata mkopo Kwa asilimia 40 huku akitoa wito kwa wakulima kuendelea kuongeza mashamba pamoja na kuiomba Serikali kuongeza wadau wengine wa sekta ya kilimo wapitie Mlango wa PASS TRUST ili wakulima waendelee kunufaika.
Mwisho.